BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

Magufuli akwama nyumbani kwake

Written By Koka Albert on Tuesday, April 3, 2012 | 7:50 AM

Dk John Magufuli
Salum Maige, Chato
SAKATA la watumishi wakiwamo watendaji wa kata na vijiji wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu Halmashauri ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, limechukua sura mpya kutokana na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, kushangazwa na kitendo cha Mkurugenzi wa halmashauri, Hamida Kwikwega, kushindwa kuwasimamisha kazi licha ya kufikishwa mahakamani.

Watendaji hao walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu wa pembejeo za kilimo zilizotolewa na Serikali.
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ilitoa pembejeo ya ruzuku halmashauri hiyo zenye thamani ya Sh1.5 bilioni, lakini katika hali isiyo ya kwaida zaidi ya Sh1.3 bilioni zinadaiwa kuishia mifukoni mwa baadhi ya watendaji hao.

Kufuatia hali hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia kwa kushirikiana na wananchi walipaza sauti kuelezea ubadhirifu huo, Serikali ilionekana kuchukua hatua za makusudi ili kubaini wahusika na kuwafikisha kortini.
Mbali na kufikishwa kortini watuhumiwa hao wakiwamo watendaji wa vijiji 30, halmashauri imeshindwa kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi zaidi wakati kesi zao zikiendelea, huku wakituhumiwa kuwatishia maisha wananchi.

Hatua hiyo juzi ilipelekea Dk Magufuli kuishtumu ofisi ya mkurugenzi kwa kushindwa kuwasimamisha kazi watendaji hao, huku baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo akiwamo Ofisa Kilimo wa Wilaya, Dk Phales Tongora, akisimamishwa kazi baada ya kufikishwa mahakamani.

 “Ubadhirifu wa fedha za pembejeo za kilimo umeisababishia Wilaya ya Chato kuwa na jina baya sana kutokana na tamaa ya watu wachache ambao wamekuwa wakikuzunguka wewe mkurugenzi na kuhujumu uchumi wa wilaya yetu,”  alisema.
Pia, Dk Magufuli aliwanyoshea kidole madiwani kwa kushindwa kuwadhibiti watendaji ambao wamekuwa wakishindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Kikwega alikiri kuwapo kwa baadhi ya watendaji wa vijiji wanaoendelea na kazi, kwa madai anasubiri uamuzi wa mahakama.

Siri ya ushindi wa Chadema Arumeru

USHINDI wa Chadema katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata tatu za udiwani, umezidi kukiweka pabaya, CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku sababu za ushindi huo zikitajwa kuwa ni matumizi mazuri ya kasoro za chama hicho tawala katika mambo mbalimbali.

Chadema kimepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki baada ya mgombea wake, Joshua Nassari kuwashinda wenzake saba katika kinyang’anyiro hicho.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hii kwa chama cha upinzani kushinda uchaguzi mdogo katika jimbo ambalo kabla halijawa wazi kwa sababu zozote zile, lilikuwa mikononi mwa CCM.

Arumeru Mashariki limekuwa wazi tangu mwanzoni mwa mwaka huu baada ya aliyekuwa mbunge wake, Jeremia Sumari (CCM), kufariki dunia.

Nassari ameshinda kwa asilimia 54.91 wakati mpinzani wake wa karibu, Sioi Sumari wa CCM alipata asilimia 44.56 ya kura halali 60,038 zilizopigwa katika vituo 327 vya kupigia kura.

Sababu za ushindi
Chadema kiliingia katika kinyang’anyiro hicho kwa kujishusha hivyo kupata muda wa kujifunza jinsi ya kwenda kuishi na wananchi wa Arumeru kwa maana ya kufahamu lugha ya kuzungumza nao, kutambua mahitaji yao, kisha kutafuta majawabu ya kuwapa juu ya mahitaji hayo.

Kilijenga timu imara ya kuratibu kampeni zake kwa ufanisi, na jukumu hilo liliangikia kwa watu watatu, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse na Meneja mwenza wake, Vicent Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini na Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge, John Mrema ambaye alipewa jukumu la kusimamia oparesheni zote.

Nyerere pia alichukuliwa kama kete ya Chadema kuwashawishi wananchi wa Arumeru ambao wanaaminika kuwa waumini wa siasa za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kupata uthibitisho kwamba hata katika familia yake, wapo watu wa upinzani.

Licha ya CCM kutuma timu nzito ya vigogo katika kampeni zake, Mwenyekiti na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mlezi wa CCM Arusha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uratibu na Uhusiano, Stephen Wassira, Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye bado mgombea wake aliangushwa.

Hata hivyo, uchaguzi huo umefanyika wakati CCM kikiwa katika mpasuko mkubwa ambao umechangiwa na siasa za makundi. Makundi hayo ni ya vigogo wa chama hicho, ambao wanajipanga kuwania Urais mwaka 2015 na kwa sasa kila kundi linaendesha mipango wa kujiimarisha katika kila eneo muhimu kuanzia ngazi za chini.

Ishara za kushindwa
Ishara za kushindwa CCM zilianza kuonekana katika mchakato wa mwanzo wa kura za maoni ndani ya chama hicho, kwani wanachama ambao walijitokeza kugombea na kushindwa, wengi wao hawakuvunja kambi zao.

Makundi yaliyokuwa na nguvu ni yale yaliyokuwa na makada wa chama hicho, William Sarakikya, Elirehema Kaaya na Elishiria Kaaya ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM Mkoa wa Arusha.
Pia siasa za makundi ndani ya CCM Mkoa wa Arusha, ambako bado vigogo wa chama hicho, hasa Katibu wa Mkoa, Mary Chatanda na Mwenyekiti wake, Onesmo Nangole hawana uhusiano mazuri kunaelezwa kuwa ni moja ya sababu za kuanguka.

Awali, Chatanda ambaye anadaiwa kuwa na mgogoro na wana-CCM wengine wa Arusha, alitajwa kumpinga waziwazi Sioi katika kura za maoni na alimpa karata yake Sarakikya na Elishilia Kaaya ambao wote walishindwa.

Pia wanasiasa waliotumika katika kampeni za CCM katika uchaguzi huo mdogo ni moja ya mambo ambayo yalikiathiri chama hicho.

Lugha zilizokuwa zikitumiwa na baadhi yao dhidi ya viongozi wa juu wa Chadema na wabunge wake kwa mfano, alizokuwa akimwaga jukwaani, mpiga kampeni nguli wa wake, Livingstone Lusinde ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), ni moja ya mambo yanayooelezwa kuwa yalichangia kupunguza kura za mgombea wa chama hicho.

Pia kuhujumiana ndani ya chama kwa kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya mikakati ya ushindi, kiasi kikubwa kumechangia chama hicho kushindwa kwa tofauti ya zaidi ya kura 6,000.

Moja ya mambo ambayo yanadaiwa kutoka ndani ya CCM, ni siri ya kuongeza vituo vya kura, mpango wa kubadilishwa baadhi ya matokeo ya fomu za mawakala, kuingizwa kura bandia kupitia mabalozi wa nyumba kumi katika vituo mapema alfajiri na pia, kuhongwa kwa baadhi ya mawakala.

Mipango hiyo inadaiwa kukwama hata kabla ya siku ya kupiga kura hali ambayo inadaiwa kuwa iliichanganya kambi ya CCM.
Hata katika upangaji wa ratiba ya kampeni na wazungumzaji katika kampeni hizo, kunadaiwa kulikuwa na hujuma miongoni mwa wazungumzaji huku kundi moja likituhumiwa kufika katika jimbo hilo, kuhujumu kampeni kwa kutoa lugha ambazo haziwapendezi wananchi na hivyo kuwachukiza.
Sababu nyingine ni gtuhuma za ufisadi zinazowakabili baaadhi ya makada wa chama hicho. Hilo limewafanya baadhi ya wananchi kukichukia wakiamini kuwa mafisadi ambao hupigwa vita na Chadema ndiyo chanzo cha umaskini mkubwa unaowakabili Watanzania.

Kampeni

Uzinduzi wa kishindo wa kampeni za chama hicho ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star, Machi 10, mwaka huu uliashiria kwamba Chadema kilikuwa kimedhamiria kushinda.

Mbali na shamrashamra za hapa na pale, mkutano wa uzinduzi ulipanga ajenda za kampeni za chama hicho na aliyekuwa mgombea, Nassari na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe waliweka bayana kwamba suala la ardhi ni miongoni mwa mambo ambayo yatapewa umuhimu mkubwa.

Ajenda nyingine ambayo pia iliwekwa wazi na Nassari ni matatizo ya maji katika maeneo mengi ya jimbo hilo ambalo kuna chanzo kikuu cha maji kwa Miji ya Arusha na Monduli.

Ajenda hizo za ardhi, maji na nyingine pia zilibebwa na timu za kampeni wabunge wa chama hicho ambao walikuwa wakifika nyumba hadi nyumba mbali na mikutano ya hadhara vijijini.

Matumizi ya helkopta katika siku tisa za mwisho za kampeni, yalimwezesha Nassari na timu yake ya kampeni kuwafikia wananchi wengi zaidi katika muda mfupi sambamba na kuongeza hamasa kwa maana ya kuwa sehemu ya kushawishi watu kufika kwenye mikutano katika sehemu mbalimbali.

Viongozi wakuu wa Chadema, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa walikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi wa Nassari.

Kulikuwa na kila dalili kwamba viongozi hawa wanakubalika na kuaminika kwa wananchi kwani kila walipofika na kuhutubia, idadi ya watu ilikuwa kubwa na utulivu ulionekana kuwa wa hali ya juu.

Uwepo wa viongozi hao ulimwongezea nguvu kubwa mgombea wao ambaye pia alionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza akitumia lugha rahisi kuzungumzia matatizo yanayowagusa watu katika eneo husika.

Ni kama alikuwa amefanya utafiti wa kila alikokweda, kwani hotuba katika kijiji kimoja haikuwa na uhusiano na hotuba ambayo angeitoa katika kijiji kilichofuata.

Kauli za mgombea huyo kuhusu maisha duni ya watu hasa kina mama ambao wamekuwa wakitozwa ushuru kwenye magulio, kukemea uonevu unaofanywa na walowezi kwenye mashamba makubwa na kuzungumzia kwa ufasaha mahitaji mengine ya wananchi kulimfanya kueleweka kwa urahisi kwa watu wa kawaida.

Lakini pia Nassari alikwepa kuingia kwenye mitego ya kujibu tuhuma mbalimbali zilizorushwa kwake na wapinzani wake hasa CCM na mara zote alikuwa akisema: “Mimi namwachia Mungu.”

Nassari aliingia kwenye uchaguzi huo kwa mara ya pili baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010 ambako alipambana na marehemu Sumari na kupata kura zaidi ya 19,000.

Udhaifu wa CCM
Timu ya kampeni ya Chadema ilimsaidia Nassari kutumia udhaifu wa CCM katika kufanikisha malengo yake.

Siasa za matusi majukwaani ambazo baadhi ya wapiga debe wake walizitumia hazikupata majibu kutoka Chadema na badala yake, Nassari alitumia msemo: “Tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu.”

Majibu ya baadhi ya tuhuma dhidi ya Chadema na mgombea wake yaliyotolewa na watu ambao si sehemu ya chama hicho yalikijenga zaidi. Mathalan, Kanisa Katoliki lilitoa tamko kwamba halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kuhusu wizi wa fedha kama ilivyodiwa na CCM.

Mengine ni kauli ya mtoto wa kwanza wa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere kwamba Vicent Nyerere ni ndugu yao tofauti na madai ya Rais Mstaafu Mkapa kwamba hakuwahi kumfahamu, huku wazazi wake Nassari wakijitokeza jukwaani kupinga kile kilichosemwa na Wassira kwamba mgombea huyo wa Chadema hakuwa na baraka za wazazi wake kugombea nafasi hiyo.

Kauli hizo ziliwafanya makada wa CCM waonekane kuwa si wa kweli mbele ya umma na hata yaliyosema baadaye yalichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni uzushi na uongo.

Sasa CHADEMA yaja kivingine

Written By Koka Albert on Monday, April 2, 2012 | 11:38 AM

Sasa mpaka watoto wameamua kuchagua "CHADEMA" Duh!!! hii sasa kali

Chama cha Chadema chashinda uchaguzi wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki,,

Hongera  sana Mheshimiwa Mbunge Mteule Joshua Nassari

WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WAJERUHIWA KWA MAPANGA MKOANI MWANZA


Mh. SALVATORY MACHEMLI Mbunge wa Ukerewe.

MH. HIGHNESS KIWIA MBUNGE WA ILEMELA
 Wabunge wawili mmoja wa Jimbo la Ilemela na mmoja wa jimbo la Ukerewe wamepigwa mapanga na mawe usiku wa leo
kuamkia asubuhi na hii inatokana viongozi hao walikuwa huko Mwanza wakati wakitembea usiku walivamiwa na watu wasiojulikana na walipigwa mapanga na kuumizwa sana huku mbunge wa Ilemela akiwa hoi bin taabani yani ameumizwa sana

TAARIFA KUTOKA KWA ZITO
"Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa.

Hali ya ndg. Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi.

Nimezungumza na Katibu wa Bunge na ndani ya muda mfupi ndg. Kiwia atasafirishwa kupelekwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi.
Ndg. Machemuli anaendelea vizuri alitoka hospitali jana (alipata huduma ya Kwanza Sekou Toure).

Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa 'moral' authority ya kutawala.

Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi. I am so depressed" BY ZITO ZUBERI KABWE 


NASSARI MBUNGE MPYA ARUMERU MASHARIKI

   

"Moja ya Usiku Mzuri sana kwenye Historia ya chama chetu. Tumeshinda Madiwani mikoa yote nyeti na zaidi tumeshinda Ubunge Arumeru. Hakuna raha kwenye siasa kama kuongeza Mbunge katikati ya kipindi cha Bunge. Twamshukuru mola. Hongera viongozi wenzangu na wanachama wetu na watanzania kwa ujumla kwa kutupa nguvu. Its a 'snow ball effect' ! Watch our steps" Anasema Zitto Kabwe.
Hatimae Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi amemtangaza Joshua Nassari, mgombea wa CHADEMA kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Arumeru Mshariki kwa kupata jumla ya kura 32,972
Aliemfuatia  Nassari ni Sioi Summari wa CCM, aliepata kura 26,757
Jumla ya kuza zilizopigwa ni 60,038, na kura zilizoharibika ni 661.
Wagombea wa vyama vingine wamepata kura kama ifuatavyo: AFP – 139, UPDP – 18, TLP – 18, SAU – 22, NRA – 35, na DP – 77.

Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa nchini, lisifanyiwe masihara

KATIKA siku za hivi karibuni mjadala wa tatizo sugu la ajira kwa vijana umekuwa ukichukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari, warsha na maeneo ya makazi ya watu.

Mjadala huu umepamba moto kutokana na idadi kubwa ya vijana ambao wako mitaani bila kazi na hivyo hawana kipato cha aina yoyote cha kuendeleza miasha yao.

Kutokana na hali hii, vijana wa Tanzania ambao ni nguvu kazi ya taifa ni zaidi ya milioni ishirikini wanaishi maisha ya dhiki na kubahatisha kwani hata sekta ya viwanda ambayo haswa ilitakiwa kuwa mkombozi imeajiri vijana 60,000 kati ya mamilioni ambao wangependa kupata shughuli ya kufanya kwenye sekta hiyo.

Tunasema kwamba idadi hii kubwa ya vijana ambao wamemaliza darasala la saba, vyuo vya ufundi hadi vyuo vikuu nchini hawajui mustakabali wa maisha yao ya sasa na yajayo.

Sote ni shahidi kwamba kasi ya ukosefu wa ajira nchini inazidi kukua kutokana na wahitimu zaidi ya milioni moja wanaohitimu katika shule na vyuo mbalimbali nchini.

Takwimu za kwamba zaidi ya wahitimu milioni moja wanamaliza shule na vyuo mbalimbali nchini ni za mwaka 2006, hivyo tunaamini kwamba huenda idadi ya vijana wanaoingia katika soko la ajira ni kubwa  zaidi ya milioni moja kwa kuwa miaka zaidi ya sita imepita tangu utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Takwimu Nchini (NBS).

Ndio maana tunatoa wito kwa taasisi husika kufanya utafiti mpya ili kuweza kubaini ukubwa tatizo kwa lengo la kukabiliana nalo baladala ya kuanza kurushiana maneno binafsi kwa wale ambao wameliongelea.
Tunasema kwamba suala la ajira ni suala nyeti ambalo halipaswi kujibiwa kwa masihara bali linahitaji majibu fasaha ambayo yatasaidia kutafuta uvumbuzi.

Katika miezi ya hivi karibuni, tulishuhudia vijana wa Kigoma Kaskazini, wakimzonga mbunge wao Zitto Kabwe kwamba awatafutie ajira kwa kuwa wamechoka kukaa vijiweni kila kukicha. Vijana hawa wa Kigoma Kaskazini wanatoa taswira moja ambayo si vijana wote wanaokaa vijiweni wanapenda kufanya hivyo bali ni kutokana na mazingira magumu ya kupata shughuli ya kufanya.

Leo hii makampunui yakitangaza nafasi ya kazi moja, waombaji ambao wana viwango vikubwa vya elimu wanaomba zaidi ya 500 katika nafasi moja na hii ni ishara kwamba kuna watu wengi sana ambao wamesoma na kushindwa kupata ajira kwenye sekta binafsi na serikalini.

Changamoto ambayo Serikali na taasisi mbalimbali zinapaswa kukabiliana nayo ni kuweza kuanzisha viwanda vingi ambavyo vinachukua idadi kubwa ya wafanyakazi, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kukuza kilimo ambacho pia kinaweza kupunguza idadi kubwa ya vijana ambao hawana ajira.

Leo hii vijana ambao wanamaliza kozi zao katika vyuo vya kilimo hawana kazi kwa kuwa sekta hiyo haijapewa kipaumbele kikubwa na Serikali, hivyo wahitimu hao wameamua kutafuta kazi nyingine ambazo hawajasomea na si tu kwa kupenda, lakini kutokana na hali halisi ya sekta ya kilimo.

Ndio maana tusema kwamba bila sekta ya kilimo na viwanda kupata msukumo mpya wa vitendo, ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kupasuka na ni wakati muafaka sasa kuanza mjadala mkubwa wa kifaifa wa ukosefu wa ajira kwa vijana kwa lengo la kupata suluhisho.

Kwa maoni yetu, tatizo la ajira nchini ni kubwa na hivyo watu waijadili hoja hiyo kwa kina badala ya kuanza kujadili nani kasema kwani yote hayo bado hayamsaidii kijana anayeshinda siku nzima bila mlo kwa kuwa hana ajira
KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger