BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

SHINDANO LA KUMTAFUTA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012 KUFANYIKA LEO

Written By Koka Albert on Monday, October 15, 2012 | 9:34 PM


 Washiriki wa shindano la kumtafuta Mama Shujaa wa Chakula wakiwa Kijijini Bagamoyo mkoani Pwani
 Mmoja wa washiriki akizumngumza walipotembelewa na waandishi wa habari Kijijini hapo leo
 Hawa ni washiri wa Maisha Plus 2012 wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari
 Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akizungumza na washiriki wa Shindano la Maisha Plus
Washiriki wa Shindano la Mama Shuja wa Chakula 2012 wakitafakari jambo wakiwa Kijijini

SUNZU AWAPIKU TWITE, OKWI KUCHAFUKA PESA




MICHAEL MOMBURI
FELIX Sunzu wa Simba anaongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa mchezaji wa kigeni anayelipwa mshahara mkubwa zaidi, huku straika mwenzake Emmanuel Okwi akishika mkia miongoni mwa wageni wa klabu hiyo.

Wakati ukiendelea kushangaa, unapaswa kutambua kuwa Mbuyu Twite wa Yanga anaongoza katika klabu ya Yanga, huku Hamisi Kiiza ambaye ni raia wa Uganda kama Okwi akishika mkia kwa wageni wa klabu hiyo ya Jangwani.

Mwanaspoti imefanya uchunguzi kwa wachezaji wa kigeni walioko klabu kubwa za Tanzania (Simba na Yanga), Rwanda (APR na Rayon) na Kenya (AFC, Gor Mahia na Sofapaka).

SIMBA
Uchunguzi ndani ya Simba umebaini kuwa straika Mzambia Felix Sunzu analipwa Dola 3,500 (Sh.5.5 milioni) akifuatiwa na beki Komanbilli Keita wa Mali na mshambuliaji Daniel Akuffo wa Ghana ambao kila mmoja analipwa Dola 1,000 ambazo ni sawa na Sh.1.6 milioni..

Beki Mkenya, Paschal Ochieng analipwa Sh.1.2 milioni sawa na straika mpambanaji Okwi anayelipwa Dola 800 ambazo ni sawa na Sh. 1.2 milioni.

Mishahara hiyo ukiondoa wa Ochieng anayelipwa kwa fedha ya Kitanzania inaweza kuongezeka kidogo kulingana na thamani ya Dola ya Marekani kwa mwezi husika lakini bado Okwi anabaki chini miongoni mwa wachezaji wa kigeni wa Simba.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba, mshahara ni maelewano baina ya pande mbili. Ochieng, Akuffo na Keita wana deni kubwa kwa Simba kuliko ilivyo kwa Okwi na Sunzu ambao wanatisha katika kikosi cha kwanza cha Kocha Milovan Cirkovic.

Keita, Akuffo na Ochieng hawana namba kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupokwa na wazalendo walionyesha kujiamini na uwezo mkubwa wa kuisaidia timu.

Ingawa Milovan ana siri kubwa moyoni kwa atakachofanya kwenye dirisha dogo, amesisitiza kuwa bado atawapa nafasi wachezaji hao kulingana na juhudi zao.

Kwa mujibu wa hesabu hizo kwa mwezi Simba inalazimika kulipa Dola 7,300 kama mishahara peke yake kwa wachezaji wa kigeni ambazo ukizidisha kwa mwaka mzima klabu hiyo italipa fedha za Kitanzania Sh 136 milioni. Hizo hazihusishi posho za wachezaji hao timu inaposhinda pamoja na gharama nyingine za papo kwa hapo ikiwamo usafiri na nyumba.

YANGA
Mkongomani, mwenye uraia wa Rwanda, Mbuyu Twite anaongoza orodha kwa kulipwa Dola 2,500 sawa na Sh.3.8 milioni akifuatiwa na Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Yaw Berko wa Ghana wanaokinga Dola 1,500 kila mmoja ambazo ni sawa na Sh.2.4 milioni.

Straika wa Burundi, Didier Kavumbagu analipwa Dola 1,200 sawa na Sh.1.9 milioni huku Kiiza wa Uganda akishikilia nafasi ya mwisho kwa wageni kwa kulipwa Dola 1,000 ambazo ni Sh.1.6 milioni.

Tofauti na ilivyo kwa Simba, mastaa wa kigeni wa Yanga wamekuwa wakicheza karibu kila mechi na mara kadhaa wamejikuta wote wakianza ingawa bado mashabiki hawajavutiwa na kiwango cha soka kuendana na majina na uzoefu wa wachezaji hao wa kigeni.

Yanga kwa wageni watano inalazimika kuwalipa Dola 7,700 kwa mwezi ambazo ukipiga hesabu ya mwaka mzima ni Dola 92,400 ambazo ukizibadili kwa fedha za Tanzania ni Sh 145 milioni.

Gharama hizo hazihusishi pia posho, usafiri gharama ndogondogo ikiwamo tiketi za kwenda na kurudi na familia zao.

Kenya na Rwanda
APR ya Rwanda ndiyo iliyokuwa ikilipa mishahara mikubwa lakini imetimua wachezaji wote wa kigeni na kujipanga upya kwa kutumia wazalendo. Klabu nyingine zenye mashabiki wengi nchini humo za Rayon na Kiyovu zimesajili wachezaji kutoka DR Congo na Burundi lakini zinawalipa mishahara ya kawaida kama wazalendo.

Nchini Kenya, Mnyarwanda Jonas Nahimana wa AFC Leopard analipwa Ksh.80,000 sawa na Sh. 1.4 milioni ambazo ni mshahara sawa na wa Mkongomani Robert Binja wa Sofapaka.

Ivan Anguyo na Danny Serunkuma ambao ni raia wa Uganda wote wakiichezea Gor Mahia ndio wanaolipwa Ksh.70,000 ambazo ni Sh. 1.3 milioni.

Kipa Mtanzania Ivo Mapunda anayeichezea Gor Mahia naye ameongezewa mshahara na kufikia Ksh.60,000 ambazo ni Sh 1.1 milioni.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA MAHUJAJI JIJINI DAR JANA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

TANZANIA YAPATA SHUJAA MPYA


 Mh Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya TWENDE PAMOJA. Kutoka kushoto Lee Patterson, Mike Knox (Director) Wilfred Moshi, Mary Iannarelli, Fiona Macpherson na Veronica Avinou
 Mike Knox mwanzilishi wa Twende Pamoja akifanya mazungumzo na Urban Pulse
 Mwanzilishi wa Twende Pamoja Mike Knox akila pozi na Frank Eyembe wa Urban Pulse Edinburgh, Scotland
 Wilfred Moshi akipeperusha bendera ya Tanzania kileleni Mlima Everest
Wilfred Moshi safarini kuelekea kileleni.Picha zote hisani ya Wilfred Moshi na Urban Pulse
Imeandikwa na Freddy Macha kwa ushirikiano na Urban Pulse

 Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi yetu kijana Wilfred Moshi, Mbongo wa kawaida tu (anayefanya kazi ya upagazi kuwahudumia watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro), ameweka rekodi mpya ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda Everest - mlima mrefu kushinda yote duniani.
 Hivi karibuni, Moshi,   alialikwa majuma matano nchini Uingereza kutembelea shule mbalimbali za Scotland akakutana na takribani wanafunzi 5,000 .
 
Wanafunzi walitaka kufahamu namna alivyopanda mlima Everest wenye mita 8,848 (futi 29, 029). Mlima huu mgumu kuukwea kuliko yote ulimwenguni umewahi kupandwa na na watu 4,000 toka ulipoanza kufikiwa kileleni na Edmund Hillary na Sherpa Tenzig Norgay mwaka 1953. Kati ya hao 200 walifariki. Mwaka huu wanne wameshafariki wakiijaribu shughuli hii inayochukua  miezi miwili na kugharimu Dola 100,000 (Shilingi milion 157,500,000) Linganisha na mlima Kilimanjaro unaodai  siku tano na gharama (ikiwepo vifaa husika) Dola 2,000 (Shilingi milioni 3, 161).
Wilfred Moshi ni Mtanzania wa kwanza na Mwafrika wa tatu kufikia kilele cha kitendawili hiki Mei 19 2012 (kilichoitwa “Chomolungma” na wenyeji kabla ya kubatizwa jina la Everest na Waingereza enzi za ukoloni)  
Wilfred aliyezaliwa mwaka 1979 na kumaliza kidato cha sita shule ya Kilimanjaro Boys, amekuwa akipanda mlima Kilimanjaro tangu angali bado shuleni na miaka 19.
Mara baada ya kuwasili Edinburgh, Scotland alikaribishwa bungeni akakutana na Waziri wa Sheria mheshimiwa Kenneth MacAskill na viongozi wengine. Safari ilikirimiwa na shirika la “Twende Pamoja” lililoanzishwa na Mike Knox miaka 30 iliyopita. “Twende Pamoja” imejenga ushirikiano kati ya wanafunzi wa Scotland na shule 34  za Kitanzania. Ni moja  ya mashirika, watu binafsi  na wafadhili mbalimbali ulimwenguni waliochangia fedha za kumwezesha Moshi kupanda mlima Everest.
Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe vile vile alisafiri toka London kumtembelea Wilfred Moshi na kumpa heko. Umbali wa London had Scotland ni kama Dar es Salaam hadi Kigoma!
Kwanini Moshi anahusudu kupanda milima?
Ukweli sisi bado hatuoni umaana (au umuhimu) wa kupanda milima. Anasema lengo lake lilikuwa kutimiza ndoto ya Mtanzania wa kwanza kupanda Everest. Pili, upandaji milima ni moja ya njia zinazoweza kusaidia kujenga jamii kwa misaada na fadhila za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO). Tujiulize vipi alisaidiwa na watu wengi namna hiyo kuchangia fedha takikana? Tatu, Moshi amethibitisha ukiwa na moyo na jitihada unaweza kufanya lolote. Ushujaa na ushupavu wake utasaidia kuwahamasisha Watanzania kuwa ukitaka kufanya jambo lolote lile unaweza ili mradi uwe na moyo na nidhamu.
Mpanda milima mashuhuri, Mike Hamill, aliyeshakwea milima yote  mikubwa saba duniani anasema katika kitabu chake kipya (“Climbing Seven Summits”) wapanda milima ni watu wenye moyo wa kufikia malengo na kufanikiwa katika maisha yao.
 Akiwa Uingereza Moshi alipanda mlima wa Ben Nevis  mrefu kuzidi  nchi hii-  wenye mita 1,344 (futi  4, 409). Baada ya kuimudu milima mitatu sasa , Wilfred Moshi ameazimia kupanda milima  katika mabara yote 7 duniani. Anasema amebakisha milima mitano: Aconcagua ( Marekani ya Kusini ), Kosciuszko (Australia), Vinson Massif ( Antarctica) McKinley(Alaska) na  Elbrus(Urusi).
Mungu ambariki Mtanzania huyu mwenye jazba na hamasa anayetuletea sifa.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZIMA MWENGE MKOANI SHINYANGA



Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti na kikombe Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ms Margareth Nyalile ambaye Manispaa yake ilishinda nafasi ya kwanza katika kufanikisha mbio za mwenge mwaka huu. Sherehe za kuzima mwenge zilifanyika mjini Shinyanga tarehe 14.10.2012
Rais Jakaya Kikwete akipokea mwenge kutoka kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa mwaka 2012 Captain Honest Mwanossa wakati wa sherehe za kuzima mwenge zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga tarehe 14.10.2012. wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mkukangara.

Kocha Yanga ataka wabadilike

Written By Koka Albert on Friday, October 12, 2012 | 2:42 AM

KOCHA wa Yanga, Enerst Brandts amewataka wachezaji wake Nurdin Bakari na Juma Seif kubadilika huku akifunga milango kwa beki Shadrack Nsajigwa.

Brandts alisema haridhishwi na kiwango cha Nurdin na Seif Kijiko kwa sasa na kuweka bayana kwamba Nsajigwa hana nafasi kwenye kikosi chake.
Wanatakiwa kubadili uchezaji wao ili wapate nafasi  kwenye kikosi cha kwanza,รฎalisema kocha huyo.

Kuhusu hatma ya beki Nsajigwa รซFusoรญ aliachwa kwenye safari ya Kanda ya Ziwa, Brandts alisema sijaona kiwango chake, sijaona umuhimu wa  yeye kuja huku, hapa nipo na wachezaji 20.

Tangu kuanza msimu huu Nsajigwa ameshindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha Yanga baada ya kuwajiliwa kwa Mbuyu Twite na Juma Abdul.

Hivi karibuni Nsajigwa alikaririwa na vyombo vya habari akisema Yanga imesajili vijana wengi wazuri ndio maana amekosa namba kwenye kikosi hicho.
Nimewapisha vijana waweze kucheza kwani wanaonyesha uwezo mzuri, naamini kwa kikosi tulichonacho tutafanya vizuri zaidi kwenye ligi,รฎ alisema  Nsajigwa.

Mambo ya Denilson akiwa na sao paulo

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger