BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

SIMBA YAVUTWA SHATI NA WAKATA MIWA WA KAGERA NA KULAZIMISHWA SARE YA GOLI 2 KWA 2

Written By Koka Albert on Wednesday, October 17, 2012 | 10:48 PM


 Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake dhidi ya Kagera Sugar wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
 Beki wa Kagera Sugar, Salum Kanoni (kushoto) akichuano na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi
Kiungo wa Kagera Sugar, Malegesi Mwangwa akichuana na mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa
Beki wa Kagera Sugar, Amandus Nesta akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Simba, Amir Maftah katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

NSSF YAWAFIKIA WASANII WA FILAMU TANZANIA


 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akizungumza wakati wa uzinduzi wa vikundi na kulathimisha na kukabidhi kadi kwa wanachama za NSSF wanachama wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) pamoja na kutoa Cheti kwa Shirikisho hilo.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza na wasanii wa Filamu Tanzania. 
 Meneja Matibabu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza katika hafla ya kutoa kadi kwa wasanii wa Filamu Tanzania
 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza katika hafla hiyo.
 Wasanii mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo
 Wasanii waliohudhuria hafla hiyo wakijisomea jarida la NSSF kujua faida za kujiunga na mfuko huo
 Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akimkabidhi cheti cha kujiunga na NSSF, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba. Kushoto ni Mkurugenzi wa Liro, Suleiman Ling'ande. 
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akimkabidhi msanii wa Filamu, Steven Nyerere kadi ya Uanachama wa NSSF
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akimkabidhi msanii wa Filamu, Anne Costantine 'Waridi' kadi ya Uanachama wa NSSF
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akimkabidhi msanii wa Filamu, Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' kadi ya Uanachama wa NSSF
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cricentus Magori akimkabidhi msanii wa Filamu, Jacob Steven kadi ya Uanachama wa NSSF
 Baadhi ya wasanii wa Filamu wakipata baada ya kujiunga na NSSF
 Ofisa Uendeshaji wa NSSF, Kiamba Rajabu akitoa maelezo kwa wasanii wa Filamu waliokuwa wakijaza fomu za kujiunga na NSSF
 Baadhi ya wasanii wakisubiri kujiandikisha uanachama wa NSSF
 Ofisa Uendeshaji wa NSSF, Kiamba Rajabu (kulia) akitoa maelezo kwa wasanii wa Filamu waliokuwa katika hatua za kujiunga na NSSF
Ofisa Uendeshaji wa NSSF, Kiamba Rajabu akitoa maelezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na NSSF  kwa wasanii wa Filamu Tanzania.

WASHINDI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012 WAPATIKANA


 Mshindi wa kwanza wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sista Martha Mwasu kutoka mkoani Dodoma (kushoto) akiwa na zawadi baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula, 2012. Katikati ni mshindi wapili kutoka mkoani Kagera Bi. Emiliana Eligaesha, kulia ni Naibu Waziri Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba.
 Washindi watatu bora kwenye shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman akimpongeza mshindiwa kwanza wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Sista Martha Mwasu kutoka mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2012.
   Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Imani Kajula akiwapongeza washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi mashindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012.
Washiriki wa shindano la Mama wa Shujaa wa Chakula 2012 wakiwa zawadi walizokabidhiwa na Benki ya NMB baada ya shindano hilo

ASKARI APIGA PICHA ZA UTUPU

Written By Koka Albert on Monday, October 15, 2012 | 9:40 PM






Nilikuwa  busy napekua katika mitandao  kadhaa...Kusema kweli nilipatwa  na   mshangao  mkubwa  baada  ya  kuinasa  picha  ya afande live  ikizagaa katika mitandao ya  udaku......

Kwa kweli sina lolote  la  kusema  na sijui  alizipiga lini na  kwa lengo  gani.....Naamini  gazeti la AMANI  lina data  kamili.


SHINDANO LA KUMTAFUTA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012 KUFANYIKA LEO


 Washiriki wa shindano la kumtafuta Mama Shujaa wa Chakula wakiwa Kijijini Bagamoyo mkoani Pwani
 Mmoja wa washiriki akizumngumza walipotembelewa na waandishi wa habari Kijijini hapo leo
 Hawa ni washiri wa Maisha Plus 2012 wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari
 Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akizungumza na washiriki wa Shindano la Maisha Plus
Washiriki wa Shindano la Mama Shuja wa Chakula 2012 wakitafakari jambo wakiwa Kijijini

SUNZU AWAPIKU TWITE, OKWI KUCHAFUKA PESA




MICHAEL MOMBURI
FELIX Sunzu wa Simba anaongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa mchezaji wa kigeni anayelipwa mshahara mkubwa zaidi, huku straika mwenzake Emmanuel Okwi akishika mkia miongoni mwa wageni wa klabu hiyo.

Wakati ukiendelea kushangaa, unapaswa kutambua kuwa Mbuyu Twite wa Yanga anaongoza katika klabu ya Yanga, huku Hamisi Kiiza ambaye ni raia wa Uganda kama Okwi akishika mkia kwa wageni wa klabu hiyo ya Jangwani.

Mwanaspoti imefanya uchunguzi kwa wachezaji wa kigeni walioko klabu kubwa za Tanzania (Simba na Yanga), Rwanda (APR na Rayon) na Kenya (AFC, Gor Mahia na Sofapaka).

SIMBA
Uchunguzi ndani ya Simba umebaini kuwa straika Mzambia Felix Sunzu analipwa Dola 3,500 (Sh.5.5 milioni) akifuatiwa na beki Komanbilli Keita wa Mali na mshambuliaji Daniel Akuffo wa Ghana ambao kila mmoja analipwa Dola 1,000 ambazo ni sawa na Sh.1.6 milioni..

Beki Mkenya, Paschal Ochieng analipwa Sh.1.2 milioni sawa na straika mpambanaji Okwi anayelipwa Dola 800 ambazo ni sawa na Sh. 1.2 milioni.

Mishahara hiyo ukiondoa wa Ochieng anayelipwa kwa fedha ya Kitanzania inaweza kuongezeka kidogo kulingana na thamani ya Dola ya Marekani kwa mwezi husika lakini bado Okwi anabaki chini miongoni mwa wachezaji wa kigeni wa Simba.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba, mshahara ni maelewano baina ya pande mbili. Ochieng, Akuffo na Keita wana deni kubwa kwa Simba kuliko ilivyo kwa Okwi na Sunzu ambao wanatisha katika kikosi cha kwanza cha Kocha Milovan Cirkovic.

Keita, Akuffo na Ochieng hawana namba kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupokwa na wazalendo walionyesha kujiamini na uwezo mkubwa wa kuisaidia timu.

Ingawa Milovan ana siri kubwa moyoni kwa atakachofanya kwenye dirisha dogo, amesisitiza kuwa bado atawapa nafasi wachezaji hao kulingana na juhudi zao.

Kwa mujibu wa hesabu hizo kwa mwezi Simba inalazimika kulipa Dola 7,300 kama mishahara peke yake kwa wachezaji wa kigeni ambazo ukizidisha kwa mwaka mzima klabu hiyo italipa fedha za Kitanzania Sh 136 milioni. Hizo hazihusishi posho za wachezaji hao timu inaposhinda pamoja na gharama nyingine za papo kwa hapo ikiwamo usafiri na nyumba.

YANGA
Mkongomani, mwenye uraia wa Rwanda, Mbuyu Twite anaongoza orodha kwa kulipwa Dola 2,500 sawa na Sh.3.8 milioni akifuatiwa na Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Yaw Berko wa Ghana wanaokinga Dola 1,500 kila mmoja ambazo ni sawa na Sh.2.4 milioni.

Straika wa Burundi, Didier Kavumbagu analipwa Dola 1,200 sawa na Sh.1.9 milioni huku Kiiza wa Uganda akishikilia nafasi ya mwisho kwa wageni kwa kulipwa Dola 1,000 ambazo ni Sh.1.6 milioni.

Tofauti na ilivyo kwa Simba, mastaa wa kigeni wa Yanga wamekuwa wakicheza karibu kila mechi na mara kadhaa wamejikuta wote wakianza ingawa bado mashabiki hawajavutiwa na kiwango cha soka kuendana na majina na uzoefu wa wachezaji hao wa kigeni.

Yanga kwa wageni watano inalazimika kuwalipa Dola 7,700 kwa mwezi ambazo ukipiga hesabu ya mwaka mzima ni Dola 92,400 ambazo ukizibadili kwa fedha za Tanzania ni Sh 145 milioni.

Gharama hizo hazihusishi pia posho, usafiri gharama ndogondogo ikiwamo tiketi za kwenda na kurudi na familia zao.

Kenya na Rwanda
APR ya Rwanda ndiyo iliyokuwa ikilipa mishahara mikubwa lakini imetimua wachezaji wote wa kigeni na kujipanga upya kwa kutumia wazalendo. Klabu nyingine zenye mashabiki wengi nchini humo za Rayon na Kiyovu zimesajili wachezaji kutoka DR Congo na Burundi lakini zinawalipa mishahara ya kawaida kama wazalendo.

Nchini Kenya, Mnyarwanda Jonas Nahimana wa AFC Leopard analipwa Ksh.80,000 sawa na Sh. 1.4 milioni ambazo ni mshahara sawa na wa Mkongomani Robert Binja wa Sofapaka.

Ivan Anguyo na Danny Serunkuma ambao ni raia wa Uganda wote wakiichezea Gor Mahia ndio wanaolipwa Ksh.70,000 ambazo ni Sh. 1.3 milioni.

Kipa Mtanzania Ivo Mapunda anayeichezea Gor Mahia naye ameongezewa mshahara na kufikia Ksh.60,000 ambazo ni Sh 1.1 milioni.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA MAHUJAJI JIJINI DAR JANA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger