BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

BOMU LAWATESA CCM, POLISI.

Written By Koka Albert on Saturday, June 22, 2013 | 2:19 AM

IGP SAIDI MWEMA. 
KATIBU MKUU MPYA WA CCM ABDULRAHMAN KINANA.

MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne, umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.

Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi unaon
esha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.

“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini kwetu ?.

“Je, kama bomu lilitengenezwa China, tuangalie kama mkataba wa majukumu ya mataifa duniani kuhusu silaha, nchi hiyo inatakiwa kutoka na kauli kuhusu bomu hilo na kwa kukaa kimya maana yake wanakubaliana na maelezo ya serikali,” alisema.

Wakati maswali hayo yakionekana kuumiza vichwa vya watawala, viongozi wa CHADEMA kwa upande wao wamegoma kutoa ushahidi walionao kwa Jeshi la Polisi mpaka Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji itakayosikiliza ushahidi huo na kuendesha kesi hiyo.

Hali ya mambo ikiwa hivyo, viongozi wa CCM na wabunge wameanza kulitumia Bunge kukishambulia CHADEMA kuhusu mlipuko huo kwa lengo la kukinusuru chama chao, Tanzania Daima limedokezwa mbinu hiyo.

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, juzi bungeni walidai kuwa CHADEMA ndio wamekuwa wakihusika na vurugu zote zinazohusisha mauaji nchini.

Kauli za viongozi hao zinakuja takriban siku tano tangu Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kudai CHADEMA kiliandaa na kuratibu shambulio hilo ambalo lilitokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.

Licha ya Mwigulu kujadili jambo lililokuwa nje ya mjadala wa bajeti na linaloendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimwacha aendelee kukilaumu CHADEMA ikionekana ni mkakati rasmi wa kulinasua Jeshi la Polisi na serikali ya CCM kwenye tuhuma hizo.

Katika madai yake, Mwigulu alianza kusema kuwa jambo la usalama wa nchi hii amekuwa akiliongelea kwa haraka haraka, hivyo watu wamekuwa hawamwelewi.

“Leo naomba nilisema kwa utaratibu, jambo la usalama nimekuwa nikilisema na kuomba kama Elia aliyemwambia mtumishi wake kuwa anamwombea Mungu amfungue macho ya kimungu ili aone jinsi yeye anavyoona.

“Jambo limetokea kama hili la Arusha, nimeyaongea sana mambo haya na sasa hivi ilipotokea mimi nitasema tena na wenzetu nikiwasema mara wanasema wataenda jimboni. Nawashauri wasiende tu jimboni, bali wajenge kabisa makao makuu ya chama chao,” alisema.

Mwigulu ambaye alikuwa akishangiliwa na baadhi ya wabunge na baadhi ya mawaziri akiwemo William Lukuvi, George Mkuchika, Ghasia, Mary Nagu na wengine alisema anausema ukweli.
“Ni lazima tuwaze tuvuke mipaka, kuna mambo yanawezekana kabisa yakawa yamejificha pale. Watu wanaangalia, wanaojitoa ufahamu wanafikiria CCM inaweza kushiriki.

“Mimi niwaambie CCM, hata bila kushiriki, moja kwa moja inawekwa kwenye lawama, jambo kama hilo likitokea. Ila CCM haina ushiriki katika jambo kama hili kwa sababu ndio watu wake kupitia serikali yake inatakiwa kuwahakikishia usalama,” alisema.

Alisema kuwa ni lazima waangalie maana wengine waliojaa ushabiki linapotokea jambo wanakwenda moja kwa moja kuwa inawezekana CCM imeshiriki.

Mwigulu aliongeza kuwa lazima yaangaliwe mazingira ya nchi kwa sasa, hasa kipindi hiki ambapo wanakuja wageni wakubwa wakiwamo marais wa China na Marekani, kwamba mataifa mengine ambayo yanajua ujio wa wageni ni biashara, wanaweza kuichafua Tanzania.

“Sisi tunakimbilia tu CCM ndiyo imejaa midomoni mwa watu, lakini hoja nyingine Tanzania imekuwa kisiwa cha amani, hivi wale ambao hawatutakii mema hamjajua eneo wanaloweza wakagusa?” alihoji.

Huku akinukuu ripoti ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuhusu utekwaji wa Mwenyekiti wake, Absalom Kibanda, katibu huyo alidai CHADEMA imetajwa kuwa ndiyo inahusika na matukio hayo ya utekeaji kwa kushirikiana na maofisa usalama wasio waadilifu ili kuonesha kuwa CCM imeshindwa kuongoza na sasa inaua watu wake.

“Niliwahi kulisema hili kuwa kuna mambo mengine yanafanyika kwa hujuma na tumeziona hizo hujuma lakini watu wengine wanawahi kuamini haraka.

“Lakini hawa wenzetu kama waliwahi kumvalisha raia sare za jeshi na alihukumiwa, wanashindwaje kila wakati wanasema polisi… polisi. Tunashindwaje kuamini kama wanaweza kumvalisha mtu nguo za polisi na akafanya yale?” alihoji.

Mwigulu alisema taarifa ya Polisi Mkoa wa Morogoro kuhusu tukio la kifo cha kijana Ali Zona, kilichotokea wakati wa maandamano ya CHADEMA, zinasema chama hicho ndicho kilihusika.

“Yule kijana aliyeuawa Morogoro taarifa zilizopo hakuuawa na polisi, ni CHADEMA wao wenyewe walitoka pale wakatengeneza ile vurugu wakamfyatulia risasi ili kutengeneza kwamba serikali ya CCM inakandamiza wapinzani,” alisema.

Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi aliongeza kuwa hata video ya mauaji ya Arusha iliyowekwa kwenye mtando wa You tube inaonesha wazi kuwa yalipangwa.

“Yule aliyekuwa anachukua video eti hakushtushwa kabisa na lile bomu, aliendelea kufuatilia kama vile ni mkanda wa harusi. Iliwahi kutokea wapi mchukua video kwenye mkutano wa hadhara kitu ambacho hakikupangwa kimelipuka, kinaua watu, yeye anendelea kama anachukua ‘sendoff’?” alihoji.

Baada ya Mwigulu kumaliza, Hawa Ghasia ambaye ni mjumbe wa NEC alipewa nafasi ya kuchangia bajeti hiyo kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge, lakini naye akatumia muda mwingi kuilaumu CHADEMA kwa matukio ya vurugu nchini.

Ghasia alitumia muda huo kupanda mbegu ya ubaguzi wa kimaeneo akidai kuwa CHADEMA wamechochea vurugu Mtwara, Mwanza, Mbeya, Morogoro na sasa Arusha ili maeneo hayo yasipate maendeleo kama Mkoa wa Kilimanjaro wanakotoka baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Ghasia alisema wiki iliyopita alikuwa Kilimanjaro anakotokea Mbowe na Ndesamburo, hakuona vurugu za kuchoma matairi wala kupigwa kwa mabomu kama ilivyo Arusha.

“Jamani tuwe macho na hawa CHADEMA hawataki wawekezaji waende mikoa mingine tofauti na Kilimanjaro ndiyo maana wanahamasisha vurugu katika mikoa ya wenzao.

“Wanafanya vurugu Arusha ili watalii wagome kwenda huko, wanataka watalii wakimbilie Kilimanjaro. Jamani tusiwakubalie hawa jamaa wataliingiza taifa letu kubaya,” alisema.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji alisema kinachofanywa na CHADEMA mkoani Arusha na kwingineko kinaathiri uwekezaji kwani wawekezaji watakimbilia nchi jirani.

Nagu alisema kutokuwapo kwa wabunge wa CHADEMA kumelifanya Bunge liwe tulivu tofauti na linavyokuwa wakiwapo wabunge hao.

Katika kile kinachoonekana wabunge wa CCM walijipanga kikamilifu kukisulubu CHADEMA, kilichokosa wawakilishi, Waziri asiye na wizara maalumu, Mark Mwandosya, alitumia kauli mbalimbali za mafumbo kukinanga chama hicho cha upinzani.

Mwandosya alisema anaamini uchaguzi mkuu ujao, watu watachagua amani dhidi ya vurugu, upendo dhidi ya chuki, amani dhidi ya vita huku kwenye siasa watachagua vyama vinavyowaelekeza katika maendeleo na si vile vinavyowaelekeza katika vurugu, migogoro na machafuko.

Kutokuwepo kwa wabunge wa CHADEMA pia kumeonekana kunatoa nafuu ya mijadala ambapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mijadala mbalimbali iliyofanyika kwa siku nne imekwenda vizuri na Bunge limekuwa kama la zamani.

Wakati hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya CCM, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, juzi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanawasiliana na makachero wao kuangalia hatua za kisheria wanazoweza kuwachukulia viongozi wa CHADEMA waliogoma kutoa ushahidi.

Alisema maelezo ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa waandishi wa habari aliozungumza nao hivi karibuni ni tofauti na yale waliyoyatoa polisi, hivyo jeshi hilo litaangalia njia za kuuthibitishia umma kuwa tuhuma dhidi yao si za kweli.
CHANZO TANZANIA DAIMA.

VICHWA VYA MAGAZETI JUMAMOSI JUNI 22/ 2013.


WAZIRI MKUU ANAHAMASISHA UKIUKAJI WA KATIBA NA SHERIA: ZITTO KABWE

ZITTO KABWE AKIWA BUNGENI AKICHANGUA MOJA YA HOJA KATIKA VIKAO VYA BUNGE MJINI DODOMA HIVI KARIBUNI AMBAPO AKERWA NA NAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGI KAYANDA PINDA JUU YAKUBA KUBALI JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU ZAIDI KWA WANAOFANYA MAANDAMANO BILA KUFUATA TARATIBU NA KULETEA VURUGU HIKI NDICHO ALICHOANDIKA KATIKA UKURASA WAKE KATIKA MTANDAO.

SIKIA HIKI KISA: HAPAMWANAMKE AKILI NA KUPANGA NJAMA ZA KUMUUA MUME WAKE.

Faith Wairimu MainaBi Faith Wairimu Maina akiwa mahakamani Nairobi Juni 19, 2013. Picha/PAUL WAWERU 

Na RICHARD MUNGUTI
NJAMA ya mwanamke za kumkatizia mumewe maisha ilitubuka na sasa amejipata anakodolewa macho na kifungo cha maisha gerezani.
 
Faith Wairimu Maina,40, mkazi wa mtaa wa Zimmermann, Nairobi aliyekuwa na hasira za mkizi aliapa atamuua mumewe John Muthee Guama “kwa sababu alikuwa na mpango wa kando.“Mimi sijui kule anakopeleka pesa zake.
 
Kila siku ni mimi nanunulia watoto chakula na kugharamia mahitaji ya nyumbani. 
 
Pesa anazopata mume wangu ni za kulewa na kustarehesha  wanawake wengine,” Wairimu alimweleza hakimu mwanadamizi Bi Peter Ndwiga.
Akiendelea na kujitetea alisema, “ Nimekuwa na taabu chungu nzima. Mimi na watoto wawili wangu tumetaabika vya kutosha huku mume wangu akiendelea na maisha ya raha mstarehe.”
 
Alisema kwamba ni yeye huwalipia watoto karo kwa vile “mumewe amewatupa.”
 
Ili kufanikisha njama yake aliwakodi watu watatu wa kumuua mumewe na kuahidi kuwa angewalipa Sh200,000 bila kujua kwamba walikuwa maafisa watatu wa polisi. 
 
Waliwasiliana naye na akakubali kuwalipa malipo ya papo hapo ya Sh40,000 na makubaliano yakawa walipwe masalio baada ya kufikisha kwake mavazi ya mumewe yakiwa na damu.
 
Damu
Polisi hao waliwasiliana na mumewe mwanamke huyo, Muthee, ambaye ni muuzaji wa macadamia, na wakachukua mavazi yake na kuyalowesha damu kutoka kwa kichinjio na kuchanganya na damu ya matumbo.
 
Ushahidi huo uliwasilishwa kortini.
Kutiwa nguvuni kwa Wairimu Juni 17 kulimshtua alipogundua wanaume watatu aliopanga nao kwamba angewalipa Sh200,000 kumuua  mumewe ndipo arithi mali yake “walikuwa maafisa wa polisi kutoka kitengo cha Flying Squad.”
 
Bw Ndwiga alifahamishwa Wairimu aliota mpango huo wa kumuua mumewe baada ya kugundua alikuwa na mpango wa kando na mwanamke mwingine kwa jina Njeri Wambaa.
Hakimu Mkuu Peter Ndwiga ameamua mwanamke huyo azuiliwe rumande gereza la wanawake la Langata akisubiri kuhukumiwa Juni 28.

BALOZI IDD SEIF AMTEMBELEA SHEHA ALIEMWAGIWA TINDIKALI VISIWANI ZANZIBAR, SERIKALI YAMSAFIRISHWA KWENDA INDIA KWA KWAMATIBABU ZAIDI.

Balozi Seif Iddi amtembelea Sheha aliemwagiwa Tindikali huko Zanzibar,asafirishwa leo kwenda india kwa matibabu zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22 Mei 2013.

Sheha Kidevu alikuwa akipatiwa huduma ya matibabu katika Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi mmoja baada ya tukio hilo.
 
Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa SMZ kwa kufanikisha safari yake ya kwenda matibabuni Nchini India mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari hiyo.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar kuelekea Nchini India kwa ajili ya Uchunguz na matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013.
 
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
 
Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya shirika la ndege la Oman kwa kupitia Muscut na amewasili Mjini Chenai Nchini India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa 12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari wake.
 
Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha Mohd Kidevu safari ya mafanikio itakayomletea hafaja njema.
 
Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa maumivu makali yenye kuchoma kama moto.
 
Sheha huyo wa Shehia yaTomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza kupatamatumainikufuatiajicho lake.
 
kuanzakuonaingawabadoanakabiliwanamaumivukatikasehemuyakeyausoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma za matibabu.
 
Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu ya afya yake hadi atakapopata nafuu na kurejea nyumbani kuendelea na harakati zake za kimaisha kama kawaida.
 
Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari yake ambayo imempa faraja kubwa.
 
Sheha Kidevu alisema maumivu yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo kufuatia huduma za karibu alizokuwa akipatiwa na madaktari wanaomuhudumia.
 
Akizungumza na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi karibuni wakati alipomkagua sheha huyo kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari kwa Binaadamu.
 
Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.
 
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa kufuatilia matukio hayo na kamwe haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo wa sheria wale wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.
 
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la kumwagiwa watu tindili kali ndan ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA UDSM

Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.

Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.

Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.

Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo.Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.

Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).

Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

LEMA ASHINDA RUFAA YAKE NA SASA KUENDELEA NA UBUNGE TENA WA JIMBO LA ARUSHA

Written By Koka Albert on Thursday, December 20, 2012 | 11:35 PM

Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Jimbo la Arusha Akiongea na wafuasi wa Chadema na baadhi ya wananchi waliojitokeza kusikiliza hukumu ya kesi yake mara baada ya kushinda rufaa yake leo katika Mahamaka Kuu 
..............................................
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema ameshinda rufaa yake ambayo ilikua inasikilizwa leo katika Mahakama Kuu. Ambapo Kesi ya kupinga ubunge wake ilifunguliwa na makada wa tatu wa CCM ambapo awali waliweza kumvua ubunge Lema Kwa Kushinda Kesi hiyo iliyotolewa Hukumu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Baadae Lema alikata Rufaa kupitia kwa wakili wake Tundu Lisu huku wakiokatiwa rufaa wakiwa na wakili wao Alute ambaye ni kaka yake Tundu Lisu.

Rufaa hii imechukua sura mpya baada ya Wakili wa Upande wa Utetezi Ambaye ni Mh Tundu Lisu akiwa ni mdogo wa damu kwa Wakili wa Waliokatiwa Rufaa Mh Alute, Hapa Ndipo palipovuta hisia za watu wengi ukizingatiwa ilikua kama Mechi kati ya CCM na Chadema huku Kaka na Mdogo Wake Wakipambana Vikali....

Huku Dk Slaa naye akimpatia PONGEZI ZAKE akiwa ameandika katika page yake ya Facebook


KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger