BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

RAIA WA AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA UJIO WA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.

Written By Koka Albert on Saturday, June 29, 2013 | 3:23 AM

Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2.

Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28
 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28. 
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP
Source:Mpekuzi blog 

MSANII LADY JAYDEE AANZISHA BIFU JIPYA NA FAtuma.

Written By Koka Albert on Saturday, June 22, 2013 | 8:41 AM

msanii wa kizazi kipya Lady Jadee akiwa ameweka pozi huku akitafakari jambo, msanii huyu ameanzisha bifu na Fatuma lakini bado hajaweka wazi Fatuma huyu ni yupi. 

Fuatilia hapa chini Jaydee anamweleza lakini kwa mafumbo, na wenye kujua watajua na wale mwenzangu na mimi tutaabaki bila jibu.












TUNAOMBA RADHI: MVULANA NA MSICHANA WAJINYONGA HADI KUFA BAADA YA WAZAZI KUKATAA WASIOANE


Mkasa huu umetokea huko Congo.
 
Wapenzi hawa wawili waliamua kuchukua jukuma la kujinyonga kwa kujininginiza kwenye mti hadi kufa baada ya wazazi wa mvulana kukataa mtoto wao asimuoe msichana huyo.
 
Baada ya jitihada zao za kuwashawishi kushindikana basi waliamua kuchukua hatua hiyo ya kujinyonga....Wazazi tuwe makini na maamuzi yetu mbele ya watoto

GARI ALILOKUWA ANASAFIRISHWA MZEE NELESON MANDELA KWENDA HOSPITALI LILIHARIBIKA.

Gari la wagongwa lililokuwa likimsafirisha hospitalini rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela wiki mbili zilizopita, liliharibika likiwa njiani kwenda hospitalini.
 
Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, amethibitisha kuwa gari hilo lilikumba na matatizo na kuwa ilibidi rais huyo wa zamani kuhamishwa hadi gari lingine.
 
Hata hivyo Bwana Maharaj, amesema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya Bwana Mandela, kwa sababu alikuwa na madaktari wa kutosha.
 
Shirika la habari la Marekani CBS limenukuu vyanzo kadhaa vikidai kuwa Mandela alisalia katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika arubaini kabla ya usaidizi kufika.
 
Shirika hilo la CBS limesema kuwa wakati Bwana Mandela alipokuwa akihamishwa hadi gari lingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
 
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alikuwa akisafirishwa kutoka hospitali moja mjini Johannesburg hadi Pretoria, wakati wa tukio hilo lililotokea tarehe nane Juni mwaka huu.
 
Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
BBC

RAIS KIKWETE WAKATI WA SHEREHE ZA MIAKA 25 YA KUTIMIZA UASKOFU WA ASKOFU TELEPHOL MKUDE MOROGORO.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Askofu mkuu wa jimbo kuu la Morogoro Telespor Mkude wakati wa maadhimisho ya sherehe ya miaka 25 ya uask
ofu wake katika viwanja vya St Peters Junior Seminary mkoani Morogoro. RAIS Jakaya Kiwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na dini wakati alipohudhuria sherehe za miaka 25 ya Askofu wa jimbo kuu la Morogoro Telesphol Mkude wa pili kulia kwa rais katika viwanja vya shule ya ST Peter mkoani Morogoro leo.

WEMA SEPETU NA UTUMIAJI WA MIKOROGO, YADAIWA YAMHARIBIA MUONEKANO WAKE.

Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri wema Sepetu ambaye ni miss Tanzania 2006. Wema ambaye umri wake bado haujamtupa , hivi sasa anakabiriwa na tatizo la ngozi kutokana na michirizi kusambaa mwili mzima hasa mapajani. 

Kamera zetu si mara ya kwanza kumshuhudia Mrembo huyu akizingirwa na uzee kwani miezi kadhaa nyuma tuliwahi andika habari inayofanana na hii lakini ikielezea zaidi michirizi ya mapajani.

Tofauti na hivyo, hivi sasa michirizi hiyo imekimbilia kifuani na mabegani hali inayoashiria kwamba siku si nyingi itahamia usoni...

"Ukweli Wema Sepetu sasa amebaki sura tu,mwili umemtupa kabisa .Nadhani hii yote inatokana na matumizi mabaya ya mikorogo"...alisema shuhuda mmoja akimtazama Wema sepetu aliyekuwa jaji katika shindano moja la umiss jijini Dar
Baada ya kumsikia shuhuda huyo akimtoa kasoro mrembo huyo, mwandishi wetu alitinga nyumbani kwa Wema Sepetu kufanya naye mahojiano juu ya jambo hili
Alipofika nyumbani hapo, mwandishi wetu aligonga geti na kufunguliwa na dada mmoja ambaye alidai kuwa maadam Wema alikuwa amelala na kwamba hawezi kuamshwa mpaka aamke mwenyewe.

BOMU LAWATESA CCM, POLISI.

IGP SAIDI MWEMA. 
KATIBU MKUU MPYA WA CCM ABDULRAHMAN KINANA.

MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne, umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.

Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi unaon
esha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.

“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini kwetu ?.

“Je, kama bomu lilitengenezwa China, tuangalie kama mkataba wa majukumu ya mataifa duniani kuhusu silaha, nchi hiyo inatakiwa kutoka na kauli kuhusu bomu hilo na kwa kukaa kimya maana yake wanakubaliana na maelezo ya serikali,” alisema.

Wakati maswali hayo yakionekana kuumiza vichwa vya watawala, viongozi wa CHADEMA kwa upande wao wamegoma kutoa ushahidi walionao kwa Jeshi la Polisi mpaka Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji itakayosikiliza ushahidi huo na kuendesha kesi hiyo.

Hali ya mambo ikiwa hivyo, viongozi wa CCM na wabunge wameanza kulitumia Bunge kukishambulia CHADEMA kuhusu mlipuko huo kwa lengo la kukinusuru chama chao, Tanzania Daima limedokezwa mbinu hiyo.

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, juzi bungeni walidai kuwa CHADEMA ndio wamekuwa wakihusika na vurugu zote zinazohusisha mauaji nchini.

Kauli za viongozi hao zinakuja takriban siku tano tangu Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kudai CHADEMA kiliandaa na kuratibu shambulio hilo ambalo lilitokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.

Licha ya Mwigulu kujadili jambo lililokuwa nje ya mjadala wa bajeti na linaloendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimwacha aendelee kukilaumu CHADEMA ikionekana ni mkakati rasmi wa kulinasua Jeshi la Polisi na serikali ya CCM kwenye tuhuma hizo.

Katika madai yake, Mwigulu alianza kusema kuwa jambo la usalama wa nchi hii amekuwa akiliongelea kwa haraka haraka, hivyo watu wamekuwa hawamwelewi.

“Leo naomba nilisema kwa utaratibu, jambo la usalama nimekuwa nikilisema na kuomba kama Elia aliyemwambia mtumishi wake kuwa anamwombea Mungu amfungue macho ya kimungu ili aone jinsi yeye anavyoona.

“Jambo limetokea kama hili la Arusha, nimeyaongea sana mambo haya na sasa hivi ilipotokea mimi nitasema tena na wenzetu nikiwasema mara wanasema wataenda jimboni. Nawashauri wasiende tu jimboni, bali wajenge kabisa makao makuu ya chama chao,” alisema.

Mwigulu ambaye alikuwa akishangiliwa na baadhi ya wabunge na baadhi ya mawaziri akiwemo William Lukuvi, George Mkuchika, Ghasia, Mary Nagu na wengine alisema anausema ukweli.
“Ni lazima tuwaze tuvuke mipaka, kuna mambo yanawezekana kabisa yakawa yamejificha pale. Watu wanaangalia, wanaojitoa ufahamu wanafikiria CCM inaweza kushiriki.

“Mimi niwaambie CCM, hata bila kushiriki, moja kwa moja inawekwa kwenye lawama, jambo kama hilo likitokea. Ila CCM haina ushiriki katika jambo kama hili kwa sababu ndio watu wake kupitia serikali yake inatakiwa kuwahakikishia usalama,” alisema.

Alisema kuwa ni lazima waangalie maana wengine waliojaa ushabiki linapotokea jambo wanakwenda moja kwa moja kuwa inawezekana CCM imeshiriki.

Mwigulu aliongeza kuwa lazima yaangaliwe mazingira ya nchi kwa sasa, hasa kipindi hiki ambapo wanakuja wageni wakubwa wakiwamo marais wa China na Marekani, kwamba mataifa mengine ambayo yanajua ujio wa wageni ni biashara, wanaweza kuichafua Tanzania.

“Sisi tunakimbilia tu CCM ndiyo imejaa midomoni mwa watu, lakini hoja nyingine Tanzania imekuwa kisiwa cha amani, hivi wale ambao hawatutakii mema hamjajua eneo wanaloweza wakagusa?” alihoji.

Huku akinukuu ripoti ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuhusu utekwaji wa Mwenyekiti wake, Absalom Kibanda, katibu huyo alidai CHADEMA imetajwa kuwa ndiyo inahusika na matukio hayo ya utekeaji kwa kushirikiana na maofisa usalama wasio waadilifu ili kuonesha kuwa CCM imeshindwa kuongoza na sasa inaua watu wake.

“Niliwahi kulisema hili kuwa kuna mambo mengine yanafanyika kwa hujuma na tumeziona hizo hujuma lakini watu wengine wanawahi kuamini haraka.

“Lakini hawa wenzetu kama waliwahi kumvalisha raia sare za jeshi na alihukumiwa, wanashindwaje kila wakati wanasema polisi… polisi. Tunashindwaje kuamini kama wanaweza kumvalisha mtu nguo za polisi na akafanya yale?” alihoji.

Mwigulu alisema taarifa ya Polisi Mkoa wa Morogoro kuhusu tukio la kifo cha kijana Ali Zona, kilichotokea wakati wa maandamano ya CHADEMA, zinasema chama hicho ndicho kilihusika.

“Yule kijana aliyeuawa Morogoro taarifa zilizopo hakuuawa na polisi, ni CHADEMA wao wenyewe walitoka pale wakatengeneza ile vurugu wakamfyatulia risasi ili kutengeneza kwamba serikali ya CCM inakandamiza wapinzani,” alisema.

Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi aliongeza kuwa hata video ya mauaji ya Arusha iliyowekwa kwenye mtando wa You tube inaonesha wazi kuwa yalipangwa.

“Yule aliyekuwa anachukua video eti hakushtushwa kabisa na lile bomu, aliendelea kufuatilia kama vile ni mkanda wa harusi. Iliwahi kutokea wapi mchukua video kwenye mkutano wa hadhara kitu ambacho hakikupangwa kimelipuka, kinaua watu, yeye anendelea kama anachukua ‘sendoff’?” alihoji.

Baada ya Mwigulu kumaliza, Hawa Ghasia ambaye ni mjumbe wa NEC alipewa nafasi ya kuchangia bajeti hiyo kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge, lakini naye akatumia muda mwingi kuilaumu CHADEMA kwa matukio ya vurugu nchini.

Ghasia alitumia muda huo kupanda mbegu ya ubaguzi wa kimaeneo akidai kuwa CHADEMA wamechochea vurugu Mtwara, Mwanza, Mbeya, Morogoro na sasa Arusha ili maeneo hayo yasipate maendeleo kama Mkoa wa Kilimanjaro wanakotoka baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Ghasia alisema wiki iliyopita alikuwa Kilimanjaro anakotokea Mbowe na Ndesamburo, hakuona vurugu za kuchoma matairi wala kupigwa kwa mabomu kama ilivyo Arusha.

“Jamani tuwe macho na hawa CHADEMA hawataki wawekezaji waende mikoa mingine tofauti na Kilimanjaro ndiyo maana wanahamasisha vurugu katika mikoa ya wenzao.

“Wanafanya vurugu Arusha ili watalii wagome kwenda huko, wanataka watalii wakimbilie Kilimanjaro. Jamani tusiwakubalie hawa jamaa wataliingiza taifa letu kubaya,” alisema.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji alisema kinachofanywa na CHADEMA mkoani Arusha na kwingineko kinaathiri uwekezaji kwani wawekezaji watakimbilia nchi jirani.

Nagu alisema kutokuwapo kwa wabunge wa CHADEMA kumelifanya Bunge liwe tulivu tofauti na linavyokuwa wakiwapo wabunge hao.

Katika kile kinachoonekana wabunge wa CCM walijipanga kikamilifu kukisulubu CHADEMA, kilichokosa wawakilishi, Waziri asiye na wizara maalumu, Mark Mwandosya, alitumia kauli mbalimbali za mafumbo kukinanga chama hicho cha upinzani.

Mwandosya alisema anaamini uchaguzi mkuu ujao, watu watachagua amani dhidi ya vurugu, upendo dhidi ya chuki, amani dhidi ya vita huku kwenye siasa watachagua vyama vinavyowaelekeza katika maendeleo na si vile vinavyowaelekeza katika vurugu, migogoro na machafuko.

Kutokuwepo kwa wabunge wa CHADEMA pia kumeonekana kunatoa nafuu ya mijadala ambapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mijadala mbalimbali iliyofanyika kwa siku nne imekwenda vizuri na Bunge limekuwa kama la zamani.

Wakati hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya CCM, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, juzi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanawasiliana na makachero wao kuangalia hatua za kisheria wanazoweza kuwachukulia viongozi wa CHADEMA waliogoma kutoa ushahidi.

Alisema maelezo ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa waandishi wa habari aliozungumza nao hivi karibuni ni tofauti na yale waliyoyatoa polisi, hivyo jeshi hilo litaangalia njia za kuuthibitishia umma kuwa tuhuma dhidi yao si za kweli.
CHANZO TANZANIA DAIMA.
KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger