BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

Karibu St John's Town Center

Written By Koka Albert on Tuesday, November 13, 2012 | 1:29 AM


ST JOHN'S TOWN CAMPUS

PHILIP MANGULA KUWA MAKAMU MWENYEKITI MPYA WA CCM-BARA

 Makamu Mwenyekiti Mteule wa CCM (Bara), Phili Mangula (kulia) akiungana na wanachama wengine kushangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alipoingia ukumbini wakati wa mkutano huo

Chama Cha Mapinduzi kimemteua Katibu Mkuu wake mstaafu, Philip Mangula kugombea nafasi ya Makamu Mwemnyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa Zanzibar akiteuliwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Uteulzi wa wagombea hao umefanywa na Kikao Cha CC na Kuthinishwa na NEC usiku wa kuamkia leo, LKatibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema leo mjini Dodoma.

Mangula na Dk. Sheni watapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu, unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma.

BENDI YA MSONDO NGOMA YAPAGAWISHA ILALA

Written By Koka Albert on Sunday, November 4, 2012 | 11:01 PM

Waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma wakitoa burudani Katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Eddo Sanga Sahani Dede na Juma Katundu bendi hiyo kila mwishoni mwa wiki utumbuiza katika ukumbi huo kwa ajili ya kutoa burudani mwishoni mwa wiki

Mpiga gila la Ridhim Wa msondo ngoma Zahoro Bangwe akizikung'uta nyuzi wakati wa onesho la bendi hiyo lililofanyika jumapili katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni

Wasanii wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe na Romani Mng'ande wakipuliza ara za mziki 

Waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma wakitoa burudani Katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Eddo Sanga Sahani Dede na Juma Katundu bendi hiyo kila mwishoni mwa wiki utumbuiza katika ukumbi huo kwa ajili ya kutoa burudani mwishoni mwa wiki.

BODI YA BAHATI NASIBU TANZANIA YATEKETEZA MASHINE ZILIZO INGIZWA NCHINI KIHOLELAMkurugezi Mkuu wa bodi ya bahati nasibu Tanzania,Abasi Tarimba akisimamia uteketezaji wa mashine za kuchezesha bahati nasibu ambazo zimeingizwa nchini bila kufuata utaratibu ambazo zimeletwa na kufungwa maeneo ya ostabay zikitokea nchini urusi ambapo nchi ya urusi imepiga marufuku mchezo wa bahati nasibu.mashine hizo zilikuwa 80 zenye thamani ya shilingi milioni 300 za kitanzania.
Mashine hizo zikiteketezwa kwa kukanyagwa na Katapila.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI MWAKA 20121.0 Utangulizi

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili mwaka 2012 unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. Idadi ya shule/vituo vilivyosajili watahiniwa mwaka 2012 ni 4,242 ikiwa ni ongezeko la vituo 55 ikilinganishwa na vile vilivyosajiliwa mwaka 2011 ambavyo vilikuwa 4,187. Kwa hiyo kwa mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 1.3.

2.0 Watahiniwa

Jumla ya watahiniwa 442,925 wamejiandikisha kufanya mtihani. Kati yao wasichana ni 214,325 (sawa na asilimia 48.39) na wavulana ni 228,600 (sawa na asilimia 51.61). 

3.0 Umuhimu wa Mtihani wa Kidato cha Pili

Mtihani wa Kidato cha Pili kama ilivyo mitihani mingine ya taifa ni muhimu sana. Matokeo ya mtihani huu hutumiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kama sehemu ya matokeo katika mtihani wa taifa wa elimu ya sekondari kidato cha nne. Mwaka huu, 2012 matokeo ya mtihani huu pia yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.

Aidha, mtahiniwa ataruhusiwa kukariri Kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi. 

4.0 Hitimisho

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza Wadau wote wa Elimu katika Kanda, Manispaa na Halmashauri za Wilaya pamoja na Wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walioandikishwa kufanya mtihani wanafanya bila kukosa.

Aidha, Wazazi, Walezi, Walimu na jamii kwa ujumla wanashauriwa kuwaandaa vema wanafunzi ili kuepukana na udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu na sheria za uendeshaji wa mitihani. 

Nawatakia watahiniwa wote wa Kidato cha pili mwaka huu mafanikio mema katika mitihani yao. 

Dkt.  Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

04/11/2012
KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger