BBC-Swahili

Sample Text

Habari

Labels

Labels

Social Icons

Blog Archive

About Me

My photo
I would like to welcome all the interested people to join the blog and together we help each other to reach our goals.

Featured Posts

Designed by Edservant. Powered by Blogger.

Sample Text

Latest Post

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA UMOJA WA VYUO VIKUU ELIMU YA JUU VYA AFRIKA MASHARIKI

Written By Koka Albert on Wednesday, October 31, 2012 | 4:03 AM


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine, Dkt. Charles Kitima, wakati alipokuwa akitembelea kukagua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki. 
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
 Makamu, akisikiliza maelezo kutoka kwa walimu wa Kampala University.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Mawaziri wa Afrika Mashariki, Musa Sirima, wakati wa uzinduzi wa mkutano huo leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

NMB YATOA MSAADA KUFANIKISHA SHEREHE ZA UFUNGUZI WA CHUO CHA NELSON MANDELA


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Profesa Burton Mwamila kilichopo mkoani Arusha ukiwa ni mchango wa kufanikisha sherehe za ufunguzi wa Chuo hicho.

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela Profesa Burton Mwamila ili kufanikisha sherehe za ufunguzi wa Chuo hicho kilichopo mkoani Arusha. Akiangalia ni Meneja wa  Benki ya NMB tawi la Clock Tower

WANAFUNZI WALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA


Kamanda wa Operesheni Maalumwa Jeshi la Polisi, Peter Mvulla akiwa ameshika bomu la kutoa machozi aloilolichukua kutoka kwa mmoja wa wanafuzi wa Shule ya Sekondari Kimnyaki iliyopo wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. Bomu hilo lilirushwa kwa wanafunzi hao askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) bila ya kulipuka na kuwaepusha na madhara ambayo yangeweza kutokea.

AIRTEL YAWAZAWADIA 500% BONUS YA MUDA WA MAONGEZI KWA WATEJA WAKE

Written By Koka Albert on Wednesday, October 24, 2012 | 11:48 AMMkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor (katikati) pamoja Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya (kushoto)  na Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar (kulia) kwa pamoja  wakionyesha moja ya vipeperushi vya promosheni mpya ya “ Jipatie Mara “ wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi kutokana na  wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea  na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku ikiwa ni sawa na 500% bonus ya muda wa maongezi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea  na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya  wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku  . Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco. Kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar.
waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea  wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku ikiwa ni sawa na 500% bonus ya muda wa maongezi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
========  ======  =======
Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake.

·         Wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi
·         Hakuna haja ya kujiunga  kwenye “ Jipatie Mara 5”

Dar es salaam Octoba 2012 Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama “Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO  ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Airtel tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi nzima mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku promosheni hii ya “Jipatie Mara 5”.  Promosheni hii itawazawadia wateja wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo , hii ni sawa na asilimia 500 ya bonus.


”Tumefanya hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha dhamira yetu ya  kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea  aliongeza Elangalloor .”

Akifafanua juu ya promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari ameshaunganishwa katika promosheni hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa matumizi yako ya siku kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo anajipatia  nafasi  zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa maongezi.
“Jipatie Mara 5” ni promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila mteja atapata ujumbe utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha kupokea ujumbe mara atakapopokea asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa maelezo zaidi juu ya  huduma hii piga 0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma zetu”aliongeza Mallya.

Airtel inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini.  kwa kupitia huduma ya Airtel money, Airtel imewawezesha watanzania kupata  huduma za kifedha kirahisi  katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa kuthibitisha uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila makato yoyote. Vile vile Airtel imeendelea kupanua zaidi  huduma za internet kwa  kuwezesha miji zaidi ya 30 nchini kupata internet yenye  kasi ya  3.75G .

REDDS YATANGAZA ZAWADI KWA WASHINDI WA FAINALI YA REDDS MISS TZ 2012

Written By Koka Albert on Tuesday, October 23, 2012 | 8:37 PM


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Inmternational Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
 Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi wa Taji la Reddds Miss Tanzania 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY, Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Leo hii tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo
 
1)   Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
2)   Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3)   Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4)   Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5)   Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6)   Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7)   Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni  Lucy Stephano – Miss Photogenic
                          Magdalena Roy – Top Model
                          Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
 
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.

MAKATIBU WAKUU WAPYA, MKURUGENZI WA TAASISI YA KUZUIA RUSHWA WAAPISHWA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Dk.Juma Malik Akili, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar   leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Nd,Ali Khalil Mirza, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar  leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Nd,Mussa Haji Ali, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar,leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,baada ya kuwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar

UZINDUZI WA VICOBA NA MH. LOWASSA KATIKA MAONYESHO YA MIAKA KUMI YA VICOBA JIJINI DAR

Written By Koka Albert on Monday, October 22, 2012 | 2:25 AM


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala ya Chama chao hicho mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam  jana.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama wa VICOBA Tanzania.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar  es Salaam  jana .Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa na ni bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea mpaka jumamosi ijayo Oktoba 27.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akicheza muziki sambamba na Wanachama wa VICOBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Biashara ya Miaka Kumi yam Wajasilia Mali wa VICOBA tangu kuanzishwa kwakwe,iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ikiwa ni ishara ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono Wanachama wa VICOBA wakati wa kuwaaga mara baada ya kufanya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akiagana na baadhi ya Wanachama wa VICOBA mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasilia mali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akiagana na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Wanachama wa VICOBA wakijiburudisha kwa kucheza Muziki.
Maandamano ya Wanachama na Wajasiliamali wa VICOBA yakipita Mbele ya Mgeni Rasmi,ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger