Home » » Waziri Nchimbi atimuliwa na waandishi wa habari

Waziri Nchimbi atimuliwa na waandishi wa habari

Written By Koka Albert on Tuesday, September 11, 2012 | 6:52 AM

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekumbana na fadhaa ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi, wakati alipozuka bila mwaliko.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, waandishi waliandamana kuanzia kwenye ofisi za Channel Ten katikati ya jiji la Dar es Salaam na kutembea hadi katika viwanja vya Jangawani lakini walipofika mwisho wa maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.

Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ukazuka kwa waandishi dhidi ya kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo yalikuwa hayamuhusu.

"Atokee.... aondokee.... hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneo yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa waziri Nchimbi mahala hapo.

Huku akizomewa, Waziri Nchimbi alijaribu kuvumilia aibu hiyo kwa takriban dakika tano huku pengine akitumai kwamba watamruhusu kuzungumza kilichompeleka mahala hapo.

Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."

Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja na gari lake la waziri.

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walizungumza na kukemea mauaji hayo na bila ya kuuma-uma maneno walisema kwamba Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na polisi na kwamba waliohusika wote wachukuliwe hatua za kisheria.

"Waandishi na wafanyakazi wengine wanalipa kodi ilipolisi wapate magwanda, wapate bunduki, wapate mabuti na wanalipwa ili walinde raia na sio kuua raia, vitendo kama hivi havikubaliki," alisema Jesse Kwayu, mhariri mkuu wa gazeti la NIPASHE.

Mwandishi mkongwe, Masoud Sanani, aliongeza: "Waarabu wanasema 'wal kiswaswa haq' yaani 'kisasi ni haki', lakini sisi kwa busara tunasema kwamba hatuna kisasi ila tunataka mambo haya yawe mwisho, waandishi waachwe wafanye kazi zao kama askari wanavyoachwa wafanye kazi zao."

"Tumeshasikia askari akitingishwa kidogo, mtu anashitakiwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake, tunataka waandishi nao waachwe wafanye kazi yao," alisema.

Waandishi walitaka familia ya marehemu Mwangosi ilelewe na watoto wasomeshwe mpaka watakapofikia.

Miongoni mwa mabango yaliyokuwapo katika maandamano hayo yalisomeka: "Bunduki na mabomu hayatazuia kalamu zetu kuandika ukweli," "Hatuogopi vitu vizito wala vitu vya
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger