

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa
Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa
Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali usiku wa
Tarehe 22 Mei 2013.
Sheha Kidevu alikuwa akipatiwa huduma ya
matibabu katika Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi
mmoja baada ya tukio hilo.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha Omar
Said Kidevu akitoa shukrani kwa SMZ kwa kufanikisha safari yake ya
kwenda matibabuni Nchini India mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati alipokwenda kumuuga
rasmi kwa safari hiyo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya
Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar
kuelekea Nchini India kwa ajili ya Uchunguz na matibabu zaidi baada ya
kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22
Mei Mwaka huu wa 2013.
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa
huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi
Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega
pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya
shirika la ndege la Oman kwa kupitia Muscut na amewasili Mjini Chenai
Nchini India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa 12.30 za asubuhi
akiambatana na Daktari wake.
Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi
yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha Mohd Kidevu safari ya mafanikio
itakayomletea hafaja njema.
Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo
alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo
ambacho akalazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema lakini hatimae
ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa maumivu makali yenye kuchoma kama
moto.
Sheha huyo wa Shehia yaTomondo
aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba hali yake hivi sasa
inaendelea vyema na ameshaanza kupatamatumainikufuatiajicho lake.
kuanzakuonaingawabadoanakabiliwanamaumivukatikasehemuyakeyausoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati
wa kipindi hichi kigumu cha huduma za matibabu.
Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd
Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufuatilia
matibabu ya afya yake hadi atakapopata nafuu na kurejea nyumbani
kuendelea na harakati zake za kimaisha kama kawaida.
Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd
Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
jitihada zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari yake ambayo imempa
faraja kubwa.
Sheha Kidevu alisema maumivu yaliyokuwa
yakimkabili ndani ya wiki hii hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo
kufuatia huduma za karibu alizokuwa akipatiwa na madaktari
wanaomuhudumia.
Akizungumza na vyombo vya Habari nje ya
Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi karibuni wakati alipomkagua sheha huyo kwa
mara ya kwanza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivyo viovu vinavyoleta
athari kwa Binaadamu.
Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya
inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza
kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika kuendelea na harakati zao za
kimaisha za kila siku.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake
vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa kufuatilia matukio hayo na kamwe
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo
wa sheria wale wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la
kumwagiwa watu tindili kali ndan ya mkoa wa mjini Magharibi
likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu
Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil
Suleiman Soraga.
Post a Comment