Home » » SIKIA HIKI KISA: HAPAMWANAMKE AKILI NA KUPANGA NJAMA ZA KUMUUA MUME WAKE.

SIKIA HIKI KISA: HAPAMWANAMKE AKILI NA KUPANGA NJAMA ZA KUMUUA MUME WAKE.

Written By Koka Albert on Saturday, June 22, 2013 | 2:15 AM

Faith Wairimu MainaBi Faith Wairimu Maina akiwa mahakamani Nairobi Juni 19, 2013. Picha/PAUL WAWERU 

Na RICHARD MUNGUTI
NJAMA ya mwanamke za kumkatizia mumewe maisha ilitubuka na sasa amejipata anakodolewa macho na kifungo cha maisha gerezani.
 
Faith Wairimu Maina,40, mkazi wa mtaa wa Zimmermann, Nairobi aliyekuwa na hasira za mkizi aliapa atamuua mumewe John Muthee Guama “kwa sababu alikuwa na mpango wa kando.“Mimi sijui kule anakopeleka pesa zake.
 
Kila siku ni mimi nanunulia watoto chakula na kugharamia mahitaji ya nyumbani. 
 
Pesa anazopata mume wangu ni za kulewa na kustarehesha  wanawake wengine,” Wairimu alimweleza hakimu mwanadamizi Bi Peter Ndwiga.
Akiendelea na kujitetea alisema, “ Nimekuwa na taabu chungu nzima. Mimi na watoto wawili wangu tumetaabika vya kutosha huku mume wangu akiendelea na maisha ya raha mstarehe.”
 
Alisema kwamba ni yeye huwalipia watoto karo kwa vile “mumewe amewatupa.”
 
Ili kufanikisha njama yake aliwakodi watu watatu wa kumuua mumewe na kuahidi kuwa angewalipa Sh200,000 bila kujua kwamba walikuwa maafisa watatu wa polisi. 
 
Waliwasiliana naye na akakubali kuwalipa malipo ya papo hapo ya Sh40,000 na makubaliano yakawa walipwe masalio baada ya kufikisha kwake mavazi ya mumewe yakiwa na damu.
 
Damu
Polisi hao waliwasiliana na mumewe mwanamke huyo, Muthee, ambaye ni muuzaji wa macadamia, na wakachukua mavazi yake na kuyalowesha damu kutoka kwa kichinjio na kuchanganya na damu ya matumbo.
 
Ushahidi huo uliwasilishwa kortini.
Kutiwa nguvuni kwa Wairimu Juni 17 kulimshtua alipogundua wanaume watatu aliopanga nao kwamba angewalipa Sh200,000 kumuua  mumewe ndipo arithi mali yake “walikuwa maafisa wa polisi kutoka kitengo cha Flying Squad.”
 
Bw Ndwiga alifahamishwa Wairimu aliota mpango huo wa kumuua mumewe baada ya kugundua alikuwa na mpango wa kando na mwanamke mwingine kwa jina Njeri Wambaa.
Hakimu Mkuu Peter Ndwiga ameamua mwanamke huyo azuiliwe rumande gereza la wanawake la Langata akisubiri kuhukumiwa Juni 28.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger