Home » » Gari la askari polisi lakamatwa na nyara

Gari la askari polisi lakamatwa na nyara

Written By Koka Albert on Thursday, July 19, 2012 | 6:16 AM

Daniel Mjema,Moshi
 POLISI katika mji mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro, wamefanikiwa kulikamata gari aina ya Toyota Noah, linalomikiwa na askari mmoja wa polisi likiwa na shehena ya pembe za ndovu.

Taarifa za uhakika zilizopatikana jana, zilisema gari hilo linalomilikiwa na askari  polisi mwenye cheo cha koplo lilikamatwa saa 2:00 asubuhi nje kidogo ya mji wa Himo.

Ofisa mmoja mwandamizi wa polisi, aliliambia gazeti hili kuwa gari hilo lililokuwa na abiria 10, liliondoka katika mji mdogo wa Tarakea wilayani Rombo, kwenda mjini Moshi.

Alisema baaada ya kufika eneo hilo, lilisimamishwa na polisi wa kikosi cha kudhibiti magendo wakishirikiana na trafiki na lilipopekuliwa lilikutwa na vipusa hivyo.

“Hizo pembe zilikuwa kwenye mifuko ya kuhifadhidia mboea,  hivi tunavyozungumza gari limeletwa hapa kituo cha kati cha polisi na abiria waliokuwa katika gari hilo wanahojiwa,”alisema.

Wilaya ya Rombo inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Tsavo, nchini Kenya na haikufahamika  kama nyara hizo za Serikali zilitokea huko au katika hifadhi ya jirani ya Amboseli nayo ya Kenya.

Hata hivyo wakati gari hilo likikamatwa, polisi huyo anayefanya kazi katika Kituo cha Polisi cha Tarakea, hakuwamo katika gari hilo lakini baada ya kuarifiwa alitoa ushirikiano kwa polisi.

Taarifa nyingine zilisema awali polisi walikuwa wamedokezwa kuwa gari hilo lilikuwa libebe waharamiaji haramu kutoka nchini Somalia, lakini hadi kufika subuhi mtego haukufanikiwa.

Kamanda wa Polisi mkoani ilimanjaro, Robert Boaz, alikiri kuwapo kwa tukio hilo lakini akaahidi kulitolea ufafanuzi kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) kwa vile alikuwa ziarani.

“Hilo tukio lipo lakini kwa sasa niko kwenye msafara ngoja nikuandikie kwa meseji” alisema Kamanda Boaz.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger