Home » » BREAKING NEWS ....NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI JIONI HII

BREAKING NEWS ....NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI JIONI HII

Written By Koka Albert on Tuesday, August 7, 2012 | 7:06 PM

http://1.bp.blogspot.com/-a-xDU-qtjH4/UCEtZGsloXI/AAAAAAAAt8Q/F3vcDXRvg4c/s1600/NAIBU%2B2.JPG 
Wananchi wakitazama gari la naibu waziri wa Afrika Mashariki
 
 
Mzimu wa ajali kwa wabunge na viongozi wa Taifa umeendelea kushika kasi hapa nchini baada Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .

Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani."

Taarifa ambayo nimeipata kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni na tayari nimewasiliana na kamanda wa polisi wa mkoa huo na amekwenda eneo la tukuio"
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger