Home » » Ndege za Malawi zafungasha virago Ziwa Nyasa

Ndege za Malawi zafungasha virago Ziwa Nyasa

Written By Koka Albert on Thursday, August 9, 2012 | 5:20 AM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
SIKU chache baada ya Serikali kuzitaka ndege zinazozunguka Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kufanya utafiti wa mafuta kuondoka mara moja, Serikali ya Malawi imetii na kuziondoa kampuni zinazofanya kazi hiyo katika ziwa hilo.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.

Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.

Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

Jana kwa nyakati tofauti, Wakuu wa Wilaya nne zilizo mpakani mwa Tanzania na Malawi za Ileje, Mbozi, Mbeya, Kyela na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro walieleza kuwa mara baada ya kauli hizo, ndege hizo za Malawi ziliondoka na kampuni zilizokuwa zikitafiti mafuta katika Ziwa Nyasa zimeacha.
“Hapa tuko cool (tulivu) kabisa tangu zile ndege zilipoacha kuruka, tofauti na hizo kauli zinazotolewa na viongozi wa Serikali (ya Malawi),” alisema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Dk Michael Kadeghe na kuongeza:

“Hapa niko kwenye Sherehe za Nanenane na Malawi wana banda lao nimetoka kulitembelea. Hali iko shwari, tunaendelea na uhusiano kama kawaida.”
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger