Home » » Super Sport kumjaribu Bocco

Super Sport kumjaribu Bocco

Written By Koka Albert on Thursday, August 9, 2012 | 5:25 AM

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco ataondoka wiki ijayo kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa na klabu ya Super Sport ya nchini Afrika Kusini.

"Nimepata taarifa kwamba natakiwa kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini, lakini ukweli ni kwamba viongozi wangu bado hawajaniambia," alisema Bocco.

“Nasubiri kuelezwa taarifa za safari hiyo kama kweli ipo kama ambavyo nimekuwa nikisikia kwa watu mbalimbali na vyombo vya habari," alisema Bocco.

Habari kutoka chnazo cha kuaminika ndani ya klabu ya Azam, kimethibitisa taarifa za Bocco kuitwa Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio.

Bocco, mfungaji wa mabao matatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Simba, robo fainali ya Kombe la Kgame zaidi ya wiki mbili zilizopita, alionyesha kiwango cha juu kwenye michuano hiyo.

“Anakwenda kufanya majaribio, hizi ni taarifa za kweli kabisa," alisema mpashaji huyo wa habari.
Aliongeza: "Ni vigumu kuamini nayokueleza, lakini fahamu kwamba (Bocco) ana safari ya kwenda kucheza kwa majaribio nchini Afrika Kusini."

Wakati wa michuano ya Kombe la Kagame, Bocco alifunga mabao matato, na kukamatana nafasi ya tatu ya ufungaji bora.Msimu uliiopita wa Ligi Kuu Bara, Bocco aliibuka kuwa mfungaji bora baada ya kukwamisha wavuni mpira mara 18 na kuwapiku washashambuliaji, Emmanuel Okwi, Kenneth Asamoah na Davies Mwape.
Share this article :

+ comments + 1 comments

August 9, 2012 at 5:47 AM

Wish you all the best big boy

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger