
Yanga ilitwaa ubingwa wa Kombe la Kagame na kuzawadiwa Sh47mil ambazo zitagawanwa kwa wote walioshiriki kuleta ubingwa huo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Msemaji wa Yanga, Luis Sendeu alisema jana kuwa wachezaji hao watapewa fedha hizo baada ya kukamilika kwa mchakato wa nani atapata nini.
Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga wataanza mazoezi yao leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kaunda ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu na zile za BankABC baada ya mapumziko ya siku tano ya Michuano ya Kagame.
Sendeu alisema kuwa baada ya mapumziko hayo wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi la timu hiyo watajikita zaidi katika hatua nyingine ya mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu.
"Kikosi chetu kesho (leo) kinaanza tena mazoezi yake yake ya kujiandaa na Ligi Kuu kufatia benchi letu la ufundi kuwapa wachezaji wiki moja ya mapumziko mara baada kumalizika kwa michuano ya Kagame.
Katika hatua nyingine, wachezaji wa kikosi hicho Nurdin Bakari pamoja na Salum Telela wataendelea kuwa kando na kikosi hicho kutibu majeraha yao ya muda mrefu baada ya kuumia wakijiandaa na Kombe la Kagame.
Post a Comment