Home » » Usajili Yanga watua TFF

Usajili Yanga watua TFF

Written By Koka Albert on Friday, August 17, 2012 | 6:56 AM

KLABU ya Yanga jana imewasilisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), majina ya wachezaji 28 iliowasajili kwa ajili ya msimu ujao, yakiwamo pia majina ya Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, ambao Simba wanadai wana mikataba nao.
Klabu ya Simba nayo inatarajia kupeleka usajili wake, yakiwemo majina ya Yondani na Twite, beki wa kimataifa aliyekuwa akicheza timu ya APR ya Rwanda kabla ya vigogo kila mmoja kudai ni mali yake.

Katika usajili wa Yanga uliowasilishwa jana TFF mbali na jina la Yondani na Twite, pia kuna makipa Yaw Berko, Ally Mustapha na Said Mohamed.

Walinzi wa Pembeni ni Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika.
Walinzi wa kati ni Nadir Haroub, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo.

Viungo wa ulinzi ni  Athuman Idd,  Juma Seif Kijiko na Salum Telela, wakati wa pembeni ni Nizar Khalfan, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme.

Kwa upande wa viungo washambuliaji, Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari, huku washambuliaji wakiwa Said Bahanunzi, Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu na Jeryson Tegete

 Mbali na kikosi hicho pia Yanga imewasilisha majina 22 ya timu ya vijana U20 ambayo wapo pia wachezaji wa timu ya taifa Saimon Msuva na Frank Domayo ambayo majina yao yamepelekwa kwa timu ya vijana lakini wataitumikia timu hiyo kwa kucheza mechi za wakubwa.

Wengine, Geofrey Nyalusi, Yusuf Abdul, Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said.

Majina mengine kwenye orodha hiyo ni Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah, Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum na  Rehani Kibingu.

Wengine ni Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi na Kassim Jongo.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger