Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor (katikati) pamoja Mkurugenzi wa
mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar (kulia) kwa pamoja wakionyesha
moja ya vipeperushi vya promosheni mpya ya “ Jipatie Mara “ wakati wa
uzinduzi wa promosheni mpya inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara
tano ya muda wa maongezi kutokana na wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara
5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa
kiwango cha pesa watakayotumia kila siku ikiwa ni sawa na 500% bonus ya
muda wa maongezi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao
makuu ya Airtel morocco.
Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar akifafanua jambo wakati wa uzinduzi
wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel
kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel
morocco. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor
akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano
Mallya.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5”
inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango
cha pesa watakayotumia kila siku . Uzinduzi huo umefanyika leo katika
ofisi za makao makuu ya Airtel morocco. Kushoto ni Mkurugenzi wa
mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya na kulia ni Mkurugenzi wa
Masoko Cheikh Saar.
waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea wakati wa uzinduzi wa
promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata
mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku ikiwa
ni sawa na 500% bonus ya muda wa maongezi. Uzinduzi huo umefanyika leo
katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
======== ====== =======
Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake.
· Wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi
· Hakuna haja ya kujiunga kwenye “ Jipatie Mara 5”
Dar es salaam Octoba 2012 Kampuni
ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe
itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama
“Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO ya
wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam
Elangalloor alisema” Airtel tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi
nzima mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku
promosheni hii ya “Jipatie Mara 5”. Promosheni hii itawazawadia wateja
wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi
itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo
, hii ni sawa na asilimia 500 ya bonus.
”Tumefanya
hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha
dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea
aliongeza Elangalloor .”
Akifafanua
juu ya promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel
Beatrice Singano Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari
ameshaunganishwa katika promosheni hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga
simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa matumizi yako ya siku kadri
mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo anajipatia nafasi
zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa maongezi.
“Jipatie
Mara 5” ni promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila
mteja atapata ujumbe utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha
kupokea ujumbe mara atakapopokea asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa
maelezo zaidi juu ya huduma hii piga 0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma zetu”aliongeza Mallya.
Airtel
inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini. kwa kupitia huduma
ya Airtel money, Airtel imewawezesha watanzania kupata huduma za
kifedha kirahisi katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa kuthibitisha
uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha
wateja wake kutuma na kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila
makato yoyote. Vile vile Airtel imeendelea kupanua zaidi huduma za
internet kwa kuwezesha miji zaidi ya 30 nchini kupata internet yenye
kasi ya 3.75G .
Post a Comment