Home » » REDDS YATANGAZA ZAWADI KWA WASHINDI WA FAINALI YA REDDS MISS TZ 2012

REDDS YATANGAZA ZAWADI KWA WASHINDI WA FAINALI YA REDDS MISS TZ 2012

Written By Koka Albert on Tuesday, October 23, 2012 | 8:37 PM


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Inmternational Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
 Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi wa Taji la Reddds Miss Tanzania 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY, Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Leo hii tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo
 
1)   Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
2)   Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3)   Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4)   Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5)   Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6)   Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7)   Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni  Lucy Stephano – Miss Photogenic
                          Magdalena Roy – Top Model
                          Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
 
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger