Home » » Kocha Yanga ataka wabadilike

Kocha Yanga ataka wabadilike

Written By Koka Albert on Friday, October 12, 2012 | 2:42 AM

KOCHA wa Yanga, Enerst Brandts amewataka wachezaji wake Nurdin Bakari na Juma Seif kubadilika huku akifunga milango kwa beki Shadrack Nsajigwa.

Brandts alisema haridhishwi na kiwango cha Nurdin na Seif Kijiko kwa sasa na kuweka bayana kwamba Nsajigwa hana nafasi kwenye kikosi chake.
Wanatakiwa kubadili uchezaji wao ili wapate nafasi  kwenye kikosi cha kwanza,îalisema kocha huyo.

Kuhusu hatma ya beki Nsajigwa ëFusoí aliachwa kwenye safari ya Kanda ya Ziwa, Brandts alisema sijaona kiwango chake, sijaona umuhimu wa  yeye kuja huku, hapa nipo na wachezaji 20.

Tangu kuanza msimu huu Nsajigwa ameshindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha Yanga baada ya kuwajiliwa kwa Mbuyu Twite na Juma Abdul.

Hivi karibuni Nsajigwa alikaririwa na vyombo vya habari akisema Yanga imesajili vijana wengi wazuri ndio maana amekosa namba kwenye kikosi hicho.
Nimewapisha vijana waweze kucheza kwani wanaonyesha uwezo mzuri, naamini kwa kikosi tulichonacho tutafanya vizuri zaidi kwenye ligi,î alisema  Nsajigwa.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger