Home » » Aliyeondoka CCM ataka JK amtimue Waziri

Aliyeondoka CCM ataka JK amtimue Waziri

Written By Koka Albert on Tuesday, April 17, 2012 | 2:53 AM

Moses Mashalla, Arusha
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya amemshauri Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu kwa tukio la kuanguka kwa ndege ya shirika la ndege nchini (ATCL) mkoani Kigoma.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Millya ambaye sasa amekihama chama hicho tawala na kujiunga Chadema, alisema kama Rais anataka taifa lisonge mbele hana budi kujenga tabia ya kuwawajibisha watendaji wake.

Hivi karibuni ndege ya shirika hilo aina ya Dash 8 Q300 ilianguka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma wakati ikijiandaa kuruka kwenda Dar es salaam kupitia Tabora ambapo magurudumu yake yalinasa kwenye tope na kushindwa kuruka na kisha kuingia porini.

“Ni jambo la ajabu sana Rais amwajibishe mara moja huyu waziri,hafai kabisa kushika nafasi hii,”alisema Ole Milya

Akizungumza kwa hisia Millya alisisitiza kwamba ni lazima viongozi mbalimbali wa Serikali nchini wajenge tabia ya kuwajibika huku akitolea mfano wa Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipojiuzulu miaka iliyopita sanjari na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond.

Alisema Serikali haikupaswa kusubiri hadi vifo vya watu vitokee katika ajali hiyo na ndipo iwawajibishe viongozi husika huku akishauri Serikali hiyo kuwa na aibu.

“Hadi watu wafe ndio tujifunze?,ni lazima tujenga tabia ya kuwajibika mbona Rais mstaafu Mwinyi na hata mheshimiwa Lowasa walijiuzulu”alihoji mwenyekiti huyo

Hatahivyo, alienda mbali zaidi na kusema kwamba Watanzania wanapaswa kuamka na kuwawajibisha viongozi wa Serikali pindi wanapovurunda na kudai kwamba imetosha kuvumilia madudu yanayojitokeza ndani ya Serikali.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger