Home » » ‘Wajasiriamali lazima wafundishwe mbinu’

‘Wajasiriamali lazima wafundishwe mbinu’

Written By Koka Albert on Tuesday, April 3, 2012 | 8:02 AM

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimesema  upo umuhimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini kusaka maarifa na elimu kama njia ya kujiendeleza kibiashara na kufikia mafanikio.

Changamoto hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Raymond Mbilinyi mkoani Kilimanjaro baada ya kufunga mafunzo ya wajasiriamali wadogo na wa kati zaidi ya 30 kutoka katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

“Mafunzo kama haya ni muhimu katika ufanyaji biashara katika maeneo yenu ,hivyo kwa kuliona hilo tutaendelea kuwapa nguvu katika kutoa semina hizi mara kwa mara nafasi inapopatikana,” alisema Mbilinyi.
Alisema kuwa tangu kuanza mafunzo hayo jumla ya wajasiriamali 250 wamepatiwa mafunzo na mafanikio yake yameonekana na mrejesho wa kutosha umepatikana kutoka kwa wafanyabiashara wenyewe.

“Tumekuwa na ziara za mara kwa mara za kuwatembelea watu wetu, tumegundua maendeleo ni makubwa sana kutokana na aina ya mafunzo wanayopewa na TIC,” aliongeza Mbilinyi.

Alisema kuwa TIC inafarijika kutokana na kukua kwa biashara, kuongezeka kwa ufanisi na bidhaa kuwa na viwango vya juu baada ya mafunzo yanayotolewa na kituo hicho.

Alilishukuru Shirika la Maendeleo ya Biaskat la Umoja Mataifa (UNCTAD), pamoja na Sido ambao wameshirikiana nao kwa karibu wakati wa utoaji wa mafunzo hayo
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger