Home » » Hasheem mmoja wa wanaolipwa zaidi Afrika!

Hasheem mmoja wa wanaolipwa zaidi Afrika!

Written By Koka Albert on Monday, April 30, 2012 | 12:12 AM

Mgonga kikapu wa Bongo anayechezea timu ya Houston Rockets ya nchini Marekani, Hasheem Thabeet ametajwa katika orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi barani Afrika.

Thabeet katika orodha hiyo anashika nafasi ya 10 akiwa anapata mshahara wa jumla ya Euro 3,960 000 kwa mwaka huku Samuel Eto'o anayechezea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Russia akishika nafasi ya kwanza kwa kupata Euro 20,000,000 kwa mwaka.

Mchezaji wa Kenya MacDonald Mariga anayecheza nchini Italia yeye anashika nafasi ya 19 akiwa anapata Euro 1,004,000.

Pia yupo mchezaji soka wa Burundi, Saidi Ntibazinkiza anayechezea klabu ya Cracovie ya nchini Poland ambaye analipwa kiasi cha Euro 243, 000.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger