Home » » Eto'o asamehe deni Barcelona

Eto'o asamehe deni Barcelona

Written By Koka Albert on Wednesday, April 4, 2012 | 2:11 AM

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto'o ameamua kufuta kesi yake ya madai ya mabilioni ya shilingi dhidi ya

klabu yake ya zamani, Barcelona.
Eto'o alikuwa akiida klabu hiyo wakati akihama kwenda Inter Milan ya Italia.
Katika madai yake, Eto'o alitaka kulipwa kiasi cha Dola za Kimarekani 3.9milioni kama sehemu ya makubaliano alipohama

na kwenda kujiunga na Inter katika msimu wa mwaka 2009.
"Barcelona ingependa kutoa taarifa ya kumshukuru Samuel Eto'o kwa dhamira yake ya kumaliza suala lililokuwa mbele

yetu," alisema taarifa ya klabu hiyo jana jioni.
"Yeye (Samuel) alikuwa mmoja kati ya wafungaji hodari zaidi kwenye historia ya klabu."
"Klabu imefurahishwa na mchango wake mkubwa wakati wote akicheza hapa, hivyo kwa hatua aliyofikia tunapenda kumshukuru

kwa kufika uamuzi huo," ilisema zaidi taarifa ya klabu hiyo.
Nahodha hiyo wa timu ya Taifa ya Cameroon, maarufu kama 'Indomitable Lions', kwa sasa anacheza klabu tajiri ya Russia

inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini huo Anzhi Makhachkala.
Alijiunga na Inter katika utaratibu wa kubadilishana wachezaji, ambapo mwenzake Zlatan Ibrahimovic alikwenda Barca.
Ibrahimovic, nyota wa kimataifa wa Sweden kwa sasa anacheza AC Milan, ambako alikwenda kujiunga kwa ada ya Dola za

Kimarekani 61milioni, wakati Eto'o alijiunga na Inter kwa dola 26milioni.
Eto'o alifungua madai yake akitaka kulipwa asilimia 15 ya mauzo yake kwenda Inter.
Hata hivyo, Barca ilisema malipo ya asilimia 15 yalikuwa halali kwa wachezaji wale ambao uhamisho wao hakuwa nje ya

Hispania.
"Kwa kuondoka Barcelona na kwenda kucheza nje ya Hispania, ilikuwa wazi kwamba hakustahili kupata asilimia 15," ilisema

zaidi taarifa ya klabu hiyo kupitia mtandao wao wa mawasiliano.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger