Home » » DIAMOND: WEMA AMEYATAKA MWENYEWE

DIAMOND: WEMA AMEYATAKA MWENYEWE

Written By Koka Albert on Wednesday, April 4, 2012 | 5:39 AMNa Shakoor Jongo
Baada kumdhalilisha Wema Isaac Sepetu mwishoni mwa wiki iliyopita, ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (pichani) amesema kuwa mpenzi wake huyo wa zamani alijitakia mwenyewe.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko katika mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa, Wema alishindwa kusoma alama za nyakati kwani hakupaswa kunyanyuka kwenda kumtunza lakini kwa kuwa hakulifahamu hilo, ndiyo maana yakamkuta yaliyomkuta.
“Siwezi kumuomba radhi Wema,” alisema Diamond na alipoulizwa kwa nini asifanye hivyo akajibu:
“Aliyataka mwenyewe, siku hiyo mchana kuna vitu vilitokea na kabla sijaenda ukumbini so kama Wema angevikumbuka asingethubutu kufanya vile.”
MTITI ULIANZIA MBALI
Diamond anayewania Tuzo za Kili 2012 akiwa kwenye ‘kategori’ sita, alisema kuwa ishu haikuanzia pale ukumbini kwani Wema alimfuata mazoezini mchana wa siku hiyo, lakini hakuonana naye.
Alisema: “Nilipoamka asubuhi nilijiandaa na kwenda mazoezini, ghafla nilipigiwa simu na mtu nikaenda mahali, kabla sijafika huko nilipigiwa simu kuwa Wema amenifuata mazoezini, nilishangaa hivi huyu mwanamke vipi?

 “Nikamwambia aliyenipigia simu kuwa sirudi hadi aondoke na kweli sikurudi hadi Wema alipoondoka.”
KUMBE NDIYE ALIYEMCHELEWESHA KWENYE SHOO
Diamond aliendelea kutambaa na mistari kuwa baada ya jaribio lake la kumfuata ukumbini kushindikana, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, alitinga nyumbani kwake usiku akiwa ameongozana na rafiki yake wa kiume aliyemtaja kwa jina la Rommy.
“Nilimpigia simu Rommy aje nyumbani kuchukua tiketi ya kuingia kwenye shoo, nilishangaa aliponiambia kuwa Wema alimng’ng’ania na kuja naye nyumbani kwangu eti kuniomba msamaha, kiukweli alinivuruga hadi nikachelewa kwenye shoo.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger