Home » » Ajira ya watoto yakomeshwa simanjiro

Ajira ya watoto yakomeshwa simanjiro

Written By Koka Albert on Saturday, June 16, 2012 | 3:06 AM

KAMISHNA Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema kuwa tatizo la ajira kwa watoto  kwenye migodi ya Tanzanite katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro limekomeshwa.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mchwampaka alisema ajira hizo zimekomeshwa kutokana na juhudi za Wizara ya Nishati na Madini, wamiliki wa migodi na jamii katika kuizuia wachimbaji wadogo.

“Nashukuru hivi sasa kwenye migodi ya Tanzanite hakuna kabisa wachimbaji wanaowatumia watoto kuchimba madini, hivyo wameweza kuitikia katazo la kutokuwatumia 'manyoka' kuchimba madini,” alisema  Mchwampaka.

Alisema kitendo cha kuwatumikisha watoto kwenye machimbo ya madini kilikuwa kikitoa picha mbaya na sifa isiyofaa duniani akishukuru kwamba kwa sasa hakuna tena watoto wanaofanya kazi migodini.

Hata hivyo, asasi isiyo ya Serikali ya Good Hope Programme ya Mji mdogo wa Mererani kupitia Mkurugenzi wake,Dorah Mushi imetajwa kutoa mchango mkubwa katika kupiga vita ajira mbaya ya watoto  waliokuwa wakitumikishwa migodini.

Mushi aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Manyara (CCM)mwaka 2005-2010 alishiriki kikamilifu kutokomeza ajira hiyo.

Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Manyara, Arusha,Tanga na Kilimanjaro ilikumbwa na tatizo la ajira kwa watoto ambao waliacha shule na kukimbilia kufanya kazi katika migodi ya Tanzanite.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger