Home » » Wanafunzi Msimbazi waanguka hovyo

Wanafunzi Msimbazi waanguka hovyo

Written By Koka Albert on Friday, June 1, 2012 | 11:43 PM

Gedius Rwiza
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Msimbazi wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu jana wa kuanguka na kupiga kelele huku wakikimbia hovyo.Wanafunzi waliokumbwa na  ugonjwa huo ni 19.

Wanafunzi hao walikuwa wakianguka mmoja baada ya mwingine.
Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Edina Ngerageza, ugonjuwa huo ulianzia kwa wanafunzi wa kidato cha nne na kufuatiwa na wa  kidato cha tatu hadi kidato cha pili.

Alisema kabla ya hali hiyo, kulikuwa na mwanafunzi mmoja wa kiume aliyeonekana kama alikuwa amechanganyikiwa huku akiwatishia walimu.

 Alisema kitendo hicho kiliwashtua sana  walimu.
Alisema baadaye, mwanafunzi huyo alimfuata mwalimu yeye na kumshika mkono na kutishia kumpiga lakini walimu wengine waliingilia kati na kumnusuru.

“Hii ni mara ya kwanza hali hii kutokea katika shule yetu na kwa kweli tumeshangaa sana,” alisema Ngerageza.

Baadhi ya wachungaji waliofika katika shule hiyo na kutoa msaada wa maombi lakini wanafunzi walionekana kuendelea kuanguka
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger