Home » » Hii Mpya Big Brother!!!!!

Hii Mpya Big Brother!!!!!

Written By Koka Albert on Monday, June 11, 2012 | 1:35 AM

 
KUTOLEWA katika utaratibu wa kawaida kila jumapili , kujitoa na kutolewa kwa makosa mbalimbali ndio gumzo katika shindano hili mwaka huu.

Msimu huu ni tofauti kabisa na mingine iliyopita,  safari hii wameingia wawili wawili na kinachoonekana hapa wengi waliingia wakiwa hawajajiandaa kucheza game ya pamoja.

Ukiwaacha Chris na Ola kutoka Nigeria ambao walijitoa baada ya mmoja kudai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo, Waangola wao hawakuwa na sababu maalumu ya kujitoa kwao.

Wao hawakukubaliana kutoka baada ya Esperanca kudai kuwa haoni sababu ya kuendelea kuwepo katika gemu wakati hawana ushirikiano kama timu na mwenzake Seydou.

Pamoja na Seydou kutaka kuendelea kubaki, sheria za shindano lilimlazimisha kuondoka kwa kuwa inasema mlikuja wawili, mtaondoka wawili labda iamriwe vingine kwa mujibu wa uendeshaji wa shindano lakini si kwa kujitoa.

Lakini ni katika shindano hili ambapo inaonekana washiriki wanavunja sheria bila kujali na mara kwa mara wamekuwa wakiadhibiwa.

Kwa mara ya kwanza washiriki walitiana adabu kwa kurushiana makonde huku kamera 54 zikiwaangalia, ni DKB na Zainab.

Kwa mara kwanza Biggie naye alilazimishwa kufuta 'nomination' na kuomba ushauri wa wadau nini kifanyike haraka kulinusuru shindano hilo ambalo lilidumaa ghafla.

Kufuatia kuondoka kwa watu saba ndani ya siku tano, wamelifanya shindano hilo kuwa na mwelekeo usiotabirika, kwani inabidi chochote kifanyike ili kuliokoa.

Hii inamaanisha kuwa chochote kinaweza kutokea hivi sasa ikiwemo hata kuwarudisha washiriki kama Seydou na Chris au kulewa washiriki 'fake'.

Lakini huku kujitoa kwa watu kunaweza kuwapa ushindi watu wasiotarajiwa kwa kuwa inaonekana washiriki waliokuwa wanapendwa ndio waliotoka.

DKB na Zainab sio wakwanza kutolewa kwa kuvunja miiko ya shindano, waliowahi kutolewa ni pamoja na Mganda, Hannington na Mtanzania Lotus.

Msimu huu ulianza ukiwa na washiriki 35 katika nyumba zote mbili lakini sasa limebakiwa na washiriki 20 tu.
Share this article :

+ comments + 1 comments

Anonymous
June 12, 2012 at 12:10 AM

Hii kweli kali

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger