Home » » Watumia powertiller kusafirisha wagonjwa

Watumia powertiller kusafirisha wagonjwa

Written By Koka Albert on Tuesday, June 5, 2012 | 4:02 AM

Esther Mwimbula, Morogoro
WAKULIMA wadogo wa Kijiji cha Kisaki  wilayani Morogoro wameyataja matrekta madogo  aina ya ‘Power tiller’ walioyanunua kwa kilimo kuwa mkombozi kwa wagonjwa hususani  wajawazito baada kubadilishwa kuwa magari ya kuwabeba badala ya kazi ya kilimo.

Hayo yalibainishwa mjini Morogoro na baadhi ya wakazi kijijini humo wakati wakitoa mrejesho wa ulaghibishaji masuala yanayorudisha nyuma maendeleo kwa jamii kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa Serikali na wananchi wilayani humo.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Kisaki kilichopo wilayani humo, Tatu Maleta alisema kuwa vijiji hususani kijiji hicho wamekuwa wakikabiliwa na kero nyingi Iikiwamo ya kukosa usafiri wa uhakika kwa wagonjwa.

Alisema ubovu wa barabara umekuwa chanzo kikubwa cha kero hiyo na kwamba matukio ya kufariki watu kwa kukosa huduma za afya ni mengi.“Tunalazimika kutumia matrekta madogo ‘Power Tiller’kuwapeleka  wagonjwa Kituo cha Afya Duthumi kilomita zaidi ya 40’’ alisema.

Akifafanua zaidi alisema kutokana na  ugumu wa usafiri wananchi wamekuwa wakilazimika kutumia ‘Power tiller’ kwa ajili ya kuwawahisha wagonjwa kwenye kituo hicho.Aidha walisema wangependa kupata elimu inayohusiana na umuhimu wa katiba ili washiriki vema katika kutunga na iwe na manufaa zaidi katika maisha yao.

Akitoa ufafanuzi wa mfumo wa mipango ya maendeleo inavyoandaliwa na jinsi inavyowanufaisha wananchi, Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka ofisi hiyo wilayani humo, Mary Nyanje mbali na kukiri kuwapo maagizo kutoka serikalini alisema mipango mingi huanzia ngazi za vitongoji na hatimaye inapitia vijiji, kata, wilaya, mkoa na hatimaye Taifa.

Mary alisema mipango inayoanzia taifani ni ile ya kitaifa akitoa mfano wa kilimo kwanza na mingineo huku ile inayogusa maendeleo ya vijijini na vitongoji akiitaja kuwa ni pamoja na ile inayohusiana na mipango ya uboreshaji huduma za jamii kama afya, maji, shule, barabara na masoko.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger