Home » » ‘Serikali iwekeze zaidi sekta ya elimu’

‘Serikali iwekeze zaidi sekta ya elimu’

Written By Koka Albert on Friday, June 1, 2012 | 11:45 PM

brahim Yamola
SERIKALI imeshauriwa kupunguza matumizi ya kawaida katika  bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2012/13 na badala yake, ielekeze uwekezaji wake  katika maendeleo ya sekta ya elimu.

Pia imeshauriwa kuacha kuitegemeza wahisani katika utekelezaji wa bajeti hiyo na kwamba msimamo sasa uwe ni wa kutegemea zaidi vyanzo vya mapato vya ndani.

Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Elizabeth Missokia, alipokuwa akizungumza namna ya kuboresha bajeti ya Serikali katika mwaka ujao wa fedha.

Missokia alisema wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, wafanye kazi ya kubaini matumizi yasiyokuwa na tija katika bajeti ya Serikali.

“Kama tungepunguza asilimia 20 ya matumizi mengine katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika mwaka wa fedha wa 2011/12, tungeweza kupata Sh64 bilioni na kuzitenga katika bajeti ya maendeleo,” alisema Missokia na kuongeza:

Alisema fedha hizo zingeweza kutumika ujenzi wa maabara 1,280 kwa bei ya Sh50 milioni kila maabara, kwa mujibu wa mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II).

Missokia alisema tabia ya wahisani kuahidi kiwango kikubwa cha fedha na baadaye kutoa kiwango kidogo, inachangia kukwamisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

“Katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2008/9 wahisani wa maendeleo walitoa Sh27.6 badala ya Sh64 bilioni walizokuwa wameahidi kutoa,” alisema mkurugenzi huyo.


Alisema katika mwaka wa fedha wa 2009/10 wahisani walitoa Sh30.3 ambazo ni sawa na asilimia 48 ya Sh63.4 bilioni walizokuwa wameahidi kutoa.

Missokia alifafanua kuwa katika miaka ya fedha ya  2008/9 na 2009/10 wahisani hawakutoa jumla ya Sh69.5 bilioni za miradi ya maendeleo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

“Maana yake ni kuwa katika miaka hiyo shughuli mbalimbali za maendeleo katika wizara hiyo, hazikutekelezwa kama zilivyotarajiwa,” alisema Missokia.

Alisema kwa msingi huo, kuna  haja ya kubuni njia mbadala za kuiwezesha nchi  kuongeza mapato yake ya ndani na kuondoa misamaha ya kodi ambayo haina tija.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger