Home » » Yondani awashusha joto mashabiki Yanga

Yondani awashusha joto mashabiki Yanga

Written By Koka Albert on Saturday, June 23, 2012 | 8:11 AM

Sweetbert Lukonge
BEKI Kelvin Yondani ambaye amekuwa kiini cha habari katika kurasa za michezo kwa zaidi ya wiki mbili sasa, hatimaye ameanza rasmi mazoezi na klabu yake, Yanga ya jijini Dar es Salaam aliyojiunga katika uhamisho ulioleta utata toka mabingwa wa soka nchini, Simba nayo ya jijini.
Awali, Yondani alitarajia kujiunga na mazoezi ya vijana hao wa jezi za Kijani na Njano juzi, lakini hakutokea na hivyo kuleta presha kwa mashabiki wa Yanga waliojitokeza kumshuhudia kwa mara ya kwanza.

Mamia ya mashabiki wa Yanga hawakuamini macho yao walipomuaona Yondani akiwasili Makao Makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani akiwa na baadhi ya wachezaji wengine.

Kilichofuata kwa mashabiki hao baada ya kumuon Yondani, ni furaha na shangwe kutoka, ikiwa ni kielelezo tosha ya kumkubali kuja Jangwani akitoka mahasimu wao wakubwa Simba.
Shangwe za kumpokea Yondani zilikwenda sambamba nyimbo za kebei toka kwa mashabiki wa Yanga dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Adeni Rage ambaye wakati fulani aliwahi kusema: "Yondani kamwe hawezi kwenda Yanga."

Ni wazi Yondani atakuwa na mzigo mkubwa wa kuisaidia Yanga kupata mafanikio baada ya msimu huu kumaliza ligi nafasi ya tatu ikiwa ni mara ya kwanza zaidi ya miaka 20.

Yondani alivaa jezi namba tano ambayo pia alikuwa akiivaa wakati akicheza Simba, na muda wote wa mazoezi kwenye Uwanja wa Kaunda alikuwa akishangiliwa na mashabiki.

Lakini hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Yondani kushangiliwa na mashabiki wa Yanga, kwani walifanya hivyo wakati alipovaa jezi ya timu ya Taifa kwenye mchezo wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia Uwanja wa Taifa zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Mbali na kelele za kushangiliwa Yondani, pia wachezaji Ladislaus Mbogo aliyejiunga na toka Toto African ya Mwanza, Saimon Msuva (Moro United) pamoja na Frank Domayo (JKT Ruvu) nao waliziteka kelele za kishabiki.

Kocha Felix Minziro alisema anafarahishwa na uwezo ulioonyeshwa na wachezaji wake wapya hali inayomfanya kuwa na matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao.

Minziro alisema kipimo chake kikubwa cha kwanza ni michuano ya Kombe la Kagame ambayo Yanga ndiyo mabingwa watetezi.

"Usajili wetu ni mzuri, wachezaji wote wapya wameonyesha uwezo mkubwa, wanajituma na wako tayari kutekeleza majukumu yao bila maelekezo mengi," alisema Minziro.

Aidha alisema uongozi wake kwa sasa unafanya mipango ya kusajili wachezaji wawili wa kimataifa kuziba nafasi za wachezaji Davis Mwape na Kenneth Asamoah ambaye Alihamis hajaonekana kwenye mazoezi tangu Alhamisi.

Kuhusu kutoonekana kwenye mazoezi kwa mchezajiRashidi Gumbo, Minziro alisema hana taarifa zozote ingawa ilidaiwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger