Home » » TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA NI HATARI KWA TAIFA

TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA NI HATARI KWA TAIFA

Written By Koka Albert on Friday, June 8, 2012 | 8:29 AM

TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
baadhi ya vijana hutumia nguvu zao kujitafutia ajira kwa namna wanayoweza.

vijana wengi hujitafuti ridhiki kwa njia mbali mbali lakini wengi huishia kutimuliwa kwenye maeneo hayo kwa madai kuwa maeneo hayo si yao na maeneo hayo kupewa wawekezaji ambao tunaambiwa ndo wenye kutuletea maendeleo 

vijana wengi hukaa vijiweni ikiwa ni kwa kukosa shughuli ya kufanya au kukosa mitaji kwa ya kufanyia biashara si kweli kwamba wote wanao kaa vijiweni hawana elimu.

Wachunguzi wa mambo wanasema, kwa hakika ukosefu wa fursa za ajira na umaskini ni kati ya changamoto kubwa miongoni mwa vijana, lakini madai ya kutaifisha migodi pamoja na lugha zinazoashiria ubaguzi ni mambo ambayo kamwe hayawezi kuvumiliwa nchini Afrika ya Kusini, nchi ambayo imepitia vipindi vigumu vya historia yake, hadi sasa walau mafanikio yanaanza kuonekana ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.
Ule wimbo wa ajira kwa vijana unaendelea kuimbwa kila siku na sasa umekuwa kero masikioni mwa watanzania. Katika kampeni nyingi za kuwania uongozi au katika majukwaa ya kisiasa,ajenda hii imekuwa ndio mtaji kwa viongozi ili wapate kura. Ahadi nyingi zimetolewa na viongozi huku wakijua kuwa ni uongo hakuna la maana wanalolifanya kutatua hili tatizo la ukosefu wa ajira,hususani kwa vijana.
Ajira 1,000,000 zilizo ahidiwa miaka mingi iliyopita bado ni kitendawili.Kuna kipindi raisi alipokuwa anatoa hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni alisema ajira alizokuwa anazungumzia ni pale mtu anapoanzisha baa, atatoa ajira kwa vijana wale watakao kuwa wanazibua vizibo vya chupa. Ni jambo la kusikitisha mkuu wa nchi kusema neno kama hilo kwa umma wa watanzania.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger