Home » » Dogo Janja arudi Dar na Kujiunga na kundi la Watanashati

Dogo Janja arudi Dar na Kujiunga na kundi la Watanashati

Written By Koka Albert on Sunday, June 24, 2012 | 4:02 AM

Baadhi ya mashabiki wa Dogo Janja wakimsubiri Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.
..Mashabiki wakisubiri Dogo Janja awasili kutoka Arusha.
 
Dogo Janja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea jijini Arusha.
Dogo Janja akiwa kabebwa na mashabiki wake pamoja na baadhi ya wasanii wa kundi la Mtanashati.
Janja akiwa na PNC baada ya kuwasili jijini Dar.
PNC akibebwa baada ya kupoteza fahamu wakati wa shamra shamra za kumkaribisha Dogo Janja.
Mashabiki wa Dogo Janja wakiwa na mabango ya kumkaribisha.
Dogo Janja akiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya kundi la Mtanashati Entertainment.
Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja, leo amerudi jijini Dar es Salaam na kujiunga na kundi la Mtanashati Entertainment. Mwanzo Dogo Janja alikuwa kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha. Janja karudi jijini kwa ndege ya Air Tanzania na anataraji kusaini mkataba na kundi hilo la Mtanashati kuanzia sasa.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger