Home » » Kura Yanga kupigwa kwa kompyuta

Kura Yanga kupigwa kwa kompyuta

Written By Koka Albert on Tuesday, June 26, 2012 | 12:53 AM

Sosthenes Nyoni
WAKATI joto la uchaguzi wa klabu ya Yanga likizidi kupanda, Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, imesema itatumia teknolojia ya kompyuta wakati wa kupiga na kuhesabu kura.
Uchaguzi mdogo wa Yanga unaosubiriwa kwa hamu unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam Julai 15 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili alisema mpango wa matumizi ya teknolojia hiyo una lengo ya kuongeza ufanisi na kuepukana na udanganyifu.

Kaswahili, alisema iwapo zoezi hilo litafanikiwa kama wanavyotarajia, litawezeshwa kupigwa hatua muhimu ndani ya klabu hiyo."Kimsingi tumepanga kufanya uchaguzi kwa ufanisi kabisa na ili kuhakikisha hilo linafanikiwa tutatumia tekonolojia ya kompyuta," alisema Kaswahili.
"Ni utaratibu mzuri na utakaoleweka kirahisi. Wanachama watapiga kura na kisha kura hizo kuhesabiwa kwa mfumo huohuo wa Kompyuta."

Alisema msingi mkubwa wa kutumia utaratibu huo ni kuhakikisha suala la udanganyifu linakosa nafasi na pia kuharakisha zoezi lenyewe la kupiga kura.Alipoulizwa kuhusu gharama za kuandaa mfumo huo, Kaswahili alisema:"Baada ya siku chache zijazo ukinifuata nitajua gharama halisi zitakazotumia."

"Hakuna shaka hilo linawezekana kwa sababu, siku hizi siyo kama zamani kwamba kila kitu lazima kitoke Ulaya,vitu vingi sasa vinapatikana hapa kwetu," aliongeza.Kaswahili alisema kuwa, kwa kuanzia kamati yake itaboresha daftari la wapiga kura ili kujua idadi ya wanachama wanaostahili kupiga kura.

"Kwanza kabisa ni lazima tuboreshe leja, lazima tujue nani yuko hai na nani amekufa ili tupate idadi kamili wanaostahili kupiga kura," alisema Kaswahili.Uchaguzi mdogo wa Yanga unafanyika kuziba nafasi kadhaa ikiwamo ya Mwenyekiti, Makamu na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu, Llyod Nchunga alitangaza kuachia ngazi mapema mwezi huu baada ya shinikizo la muda mrefu toka baadhi ya wanachama waliomtaka kufanya hivyo.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger