Home » » Serikali yaahidi walioua mtalii kukamatwa

Serikali yaahidi walioua mtalii kukamatwa

Written By Koka Albert on Saturday, June 23, 2012 | 7:45 AM

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, wamemhakikishia Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek, kuwa majangili wote waliohusika na mauaji ya mtalii Eric Brekelmans(53) wanakamatwa.

Hatua hiyo inafuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete, kuwaagiza mawaziri hao kufuatilia mauaji hayo, hali iliyosababisha kukatisha kuhudhuria vikao juzi kwenda Arusha kukutana na Balozi Koekkoek na mjane wa Brekelmans, Annelnes.

Kifo hicho kilitokea katika Kambi ya Moivaro,Kijiji cha Robanda, kwa kupigwa risasi na majangili.
Mawaziri hao, waliondoka kwa ndege ya Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) juzi mchana mjini Dodoma kwenda Serengeti kufuatilia tukio hilo.

Pia, majangili hao walimuua Meneja msaidizi wa kambi hiyo,  Renatus  Bernard na watalii wengine 40 waliporwa mali zenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni.

Wakizungumza juzi usiku mjini Arusha na balozi huyo na mjane nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Leopard, Zuher Fazal,mawaziri hao walitoa pole kwa tukio hilo ambalo walisema siyo la kawaida na ndiyo  maana walitumwa na Rais Kikwetekwenda eneo la tukio.

Balozi Kagasheki alisema,tukio hilo limeisononesha Serikali na Watanzania kwa ujumla, kwani dunia nzima inatambua amani na utulivu uliopo nchini.

Dk Nchimbi alisemaSerikali itahakikisha wote waliohusika na mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Naye mjane Brekelmans, Annelnes aliishukuru Serikali ya Tanzania, kwa ukaribu ilioonyesha na kwamba, mumewe aliuawa kwa kupigwa risasi kifuasi wakati akipambana na majangili hayo, huku yeye akijeruhiwa kwa panga.

Hata hivyo, Annelnes alisema usalama katika kambi hiyosiyo mzuri, kwani ina eneo kubwa na hakuna usalama wa kutosha, jambo ambalo alishauri lirekebishwe.

Kwa upande wake,Balozi Dk Koekkoek alieleza kusikitishwa na tukio hilo, huku akimshukuru Rais Kikwete, mawaziri hao na watu wengine ambao wamekuwa wakishirikiana naye tangu tukio hilo kutokea.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger