Home » » Kufukuzwa kwa Dogo Janja Tip Top, Madee, Babu Tale, Dogo Janja wafunguka kisa mkasa..

Kufukuzwa kwa Dogo Janja Tip Top, Madee, Babu Tale, Dogo Janja wafunguka kisa mkasa..

Written By Koka Albert on Saturday, June 16, 2012 | 3:19 AM

Dogo Janja; Walinichukua ili wajifaidishe
Madee:Dogo hana adabu
Babu Tale: Tatizo yupo katika 'balehe'

Na Harriet Makwetta
BAADA ya msanii chipukizi wa muziki wa hiphop Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja kufunguka kuwa ameamua kuondoka Tip Top Connection kutokana dhuluma na uonevu, viongozi wa kundi hilo nao wamefunguka na kuelezea sababu zilizomfanya kijana huyo kuamua kurudi nyumbani kwao Arusha kuwa ni kubanwa.

Kwa mujibu wa mlezi wa Dogo Janja, Hamadi A. Seneda maarufu kama Madee anasema aliamua kumuita baba wa Dogo Janja mapema wakati alipoona kijana wake ameanza kuharibikiwa. Licha ya kukanywa kitabia lakini bado aliendelea kuonyesha ukaidi mpaka kufikia hatua ya kukosana na meneja wa Tip top Connection, Babu Tale.

"Si kwamba amefukuzwa, ieleweke hivyo, ila Dogo Janja ameamua kuondoka yeye mwenyewe kwa ridhaa yake, kwani tulianza kufuatilia maendeleo yake shuleni pamoja na baadhi ya mambo ambayo alikuwa akiyafanya kinyume, lakini kuona hivyo ndio akaamua kuondoka" anasema Madee.

Kuhusiana na suala la msanii huyo kunyang'anywa kadi yake ya benki na kuonekana na salio dogo la kiasi cha 25 elfu tu katika akaunti yake ya benki, pamoja na simu Madee alifunguka zaidi.

"Nilitaka kujua akaunti yake ina shilingi ngapi, lakini cha kushangaza ilikuwa na 25 elfu tu, kitu kile kilinikasirisha kwani nilijua alikuwa na fedha nyingi ambazo meneja humwekea, kadi yake anayo yeye peke yake nashangaa kama si yeye aliyekuwa akizichukua ina maana nani alikuwa akichukua? anahoji,

"Chanzo cha Dogo kuanza kukacha shule ni kulewa sifa pamoja na fedha alizokuwa akizitumia kwa mambo yasiyo na maana " anasema Madee.

 Madee anafafanua kuwa aliamua kumnyang'anya simu baada ya kuikagua na kuona meseji za kebehi na dharau alizokuwa akitumiana na rafiki yake anayeitwa Khalfan huku akimsema Madee, Babu Tale na Manecky, hivyo aliamua kuzikopi kwenye simu yake.

Naye Meneja wa Tiptop Connection, Babu Tale anasema "Unajua siwezi zungumza sana lakini mzazi yeyote anajua watoto walivyo, Dogo Janja yupo katika umri wa usumbufu hilo lipo wazi, lakini kapitiliza, hata akionywa anakuja juu" anasema.

Akizungumzia suala la malipo, Tale anasema mara nyingi shoo walikuwa wanafanya kama kundi "tulifanya shoo kwa kundi sasa kama kundi linalipwa milioni mbili, Si busara kumpa Dogo Janja fedha nyingi, hivyo tulimpa kidogo na nyingine alitumiwa baba yake na wakati mwingine aliwekewa katika akaunti yake" anasema Tale.

Madai ya Dogo Janja...
Dogo Janja anasema kilichomfanya aondoke Tip Top ni uonevu na dhuluma ambazo zilikuwa zikifanywa na watu aliowaamini.

Anasema tangu afike jiji hajawahi kusaidiwa chochote na Madee ambaye hujitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa ndiye mlezi wake.Zaidi  ya muziki, kula, malazi na ada ya shule vyote alikuwa akipatiwa na rafiki yake aitwaye Abdallah Doka na ndiko alikokuwa akiishi mtoto huyu.

Anasema kutokana na ngoma zake kuwa kali alikuwa akipata 'show' nyingi na zote alikuwa akilipwa zaidi ya shilingi milioni moja.

Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger