Home » » Duuuuuh,,, Kumbe mpaka Twiga Stars Kulikuwa na wasagaji!!!!!!!!!

Duuuuuh,,, Kumbe mpaka Twiga Stars Kulikuwa na wasagaji!!!!!!!!!

Written By Koka Albert on Thursday, June 21, 2012 | 3:21 AM

KOCHA aliyetema kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Boniface Mkwasa amesema moja ya mambo yaliyokuwa yakimchukiza na kuyakemea kwa nguvu zote ni tabia ya usagaji kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Mkwasa alitangaza kuachia ngazi kuifundisha Twiga  mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni siku moja baada ya kukosa fursa ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia kufungwa nyumbani na ugenini na wenzao wa Ethiopia.

Mkwasa, mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), alikiri kuwapo kwa vitendo hivyo kwa baadhi ya wachezaji, na waliobainika walichukuliwa hatua mara moja.
Bila kuwataja majina baadhi ya wachezaji waliokuwa na tabia hizo, Mkwasa alisema uongozi wake ulilazimika kuwatimua waliobainika kupenda mchezo huo.

Mkwasa aliyekuwa akihojiwa na kipindi cha 'Tuongee asubuhi' kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Star Tv alisema: “Kwa wale tuliokua tukiwasikia na kupata ushahidi kupenda tabia ya usagaji tuliwaondoa kwenye timu." Mkwasa alisema mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na meneja wa timu kufuatilia kwa karibu tabia za wachezaji hao.

“Nilikuwa nawasiliana na meneja wa timu na kuchukua hatua haraka kwa wale wote waliokuwa na tabia ya kupenda kusagana," alisema kocha huyo.

Wakati huohuo, mdau mkubwa wa soka la wanawake nchini na miongoni mwa waanzilishi wa ligi ya wanawake jijini Dar es Salaam, Frank Mchaki, amepongeza hatua ya aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa (Twiga Stars), Boniface Mkwasa kuachia ngazi.

Mchaki, alisema uamuzi wa Mkwasa unastahili pongezi hasa kutoka na ukweli kwamba siyo utamaduni wa wengi kukubali kuwajibika pale wanaposhindwa kufikia malengo waliyopewa.

"Nampongeza kwa uamuzi wake,  lakini Chama cha Soka la Wanawake (TWFA), ambacho ndicho chenye jukumu la kuhakikisha soka la wanawake linasonga mbele kinafanya nini,"alihoji Msaki.
Mchaki, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Kindondoni (Kifa), alisema ni ndoto kwa soka la wanawake kufanikiwa kama hakutakuwa na mpango endelevu wa kuibua vipaji vipya.

"Timu yetu ni ile ile, wachezaji ni walewale miaka nenda, rudi. Sasa katika hali kama hii, Mkwasa anaweza kuleta mabadiliko?" alihoji Mchaki.

Matokeo ya kufanya vibaya kwa Twigani kwa sababu ya kutotiliwa mkazo ligi ya wanawake ambayo ndiyo mhimili mkubwa wa kujenga timu imara ya taifa.

Alitoa ushauri kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kukaa chini na kujadili kwa pamoja nini kifanyike ili kuinua soka hilo lililoanza kuvuta hisia za mashabiki wengi.

"Kwa hali ilivyo sasa, kufikia mwaka 2015, Twiga Stars hii tunayoiona sasa haitakuwapo tena kama hakutakuwa na juhudi za haraka kutoka mamlaka zinazosimamia mchezo wa soka," alisema Mchaki.
Share this article :

+ comments + 1 comments

June 21, 2012 at 3:23 AM

kuwatimua ilikuwa jambo la maana,,,na inabidi wasaidiwe ili waweze kuacha mchezo huo kabisa,,,

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger