Home » » UCHAGUZI YANGA: 29 warudisha Fomu

UCHAGUZI YANGA: 29 warudisha Fomu

Written By Koka Albert on Thursday, June 7, 2012 | 6:52 AM

Kati ya Watu 33 waliochukua Fomu za kugombea uongozi katika Uchaguzi wa Klabu ya Yanga utakaofanyika Julai 15 kujaza nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe 9 wa Kamati ya Utendaji, Wagombea 29 tu ndio waliorudisha Fomu kabla ya kufungwa kwa zoezi hilo leo Jioni Jumatano Juni 6.

Akithibitisha habari hizo, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili, amesema ni Watu 29 ndio waliorudisha Fomu zao na nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti zina Wagombea wanne kila mmoja huku Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wapo Watu 21.

Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti ni Mfadhili mkubwa wa Yanga Yusuf Manji ambae mmoja wa Wapinzani wake kwenye kuwania wadhifa huo ni Mwanamama Sarah Ramadhani ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya sasa akiwa mmoja wa Wajumbe wanne ambao hawakujiuzulu.

Kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti yupo Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayay Tembele, ambae alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji lakini alijiuzulu Mwezi uliopita, na ambae pia anagombea nafasi ya Ujumbe.

Zoezi linalofuata ni kuhakiki Majina na Fomu za Wagombea ambazo zimerudishwa ambalo litafanywa kwa pamoja kati ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kwa kushirikiana na ile Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Yanga imelazimika kufanya Uchaguzi mdogo baada ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wake Llloyd Nchunga na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanane Mwezi uliopita na hivyo kulazimishwa na TFF kufuata Katiba kwa kufanya Uchaguzi mdogo kuziba nafasi hizo.

Pia Mjumbe mmoja alifariki Dunia na kuacha Kamati iwe na Wajumbe wanne tu waliobakia ambao ni Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia.

WAGOMBEA:
NAFASI YA MWENYEKITI NI :
1.John Poul Jembele
2.Sarah Ramadhani
3.Yusufal Manji
4.Edgar Chibula

MAKAMU MWENYEKITI:
1.Clement Sanga
2.Yono Kivela
3.Ally Mayay Tembele
4.Ayoub Nyenzi
Share this article :

+ comments + 2 comments

Anonymous
June 7, 2012 at 7:21 AM

Ndo mnazinduka kumekucha?

June 7, 2012 at 11:57 PM

Safi sana,,that what we need in our club,,sio walala njaa

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger