Home » » Brela: Wafanyabishara tafuteni taarifa zaidi

Brela: Wafanyabishara tafuteni taarifa zaidi

Written By Koka Albert on Wednesday, May 23, 2012 | 2:51 AM

Esther Mwimbula, Morogoro
 WAKALA wa Usajili Biashara na Leseni nchini (Brela), imewataka wafanyabishara kujenga tabia na utamaduni wa kupata taarifa zaidi kupitia tovuti na vipeperushi ili kuweza kutambua tofauti zilizopo kwenye biashara na kampuni na kuweza kupiga hatua za  kimaendeleo.

Naibu Msajili wa Brela,  Andrew Mkapa  aliyasema hayo jana , wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu ya usajili wa kampuni, majina ya bishara, leseni za viwanda na miliki ubunifu yanayofanyika mjini hapa.

Mkapa alisema , wapo watu wanaochanganya jina la biashara na kusema, wanamiliki kampuni jambo ambalo halileti maana na wakati mwingine linawarudisha nyuma kimaendeleo kwa kujiona wana kampuni kubwa nyingi huku kampuni  ikiwa ni moja tu.

Alisema, kupata taarifa kwenye tovuti mbalimbali kutawasaidia wafanyabiashara waliowengi kutambua mengi zaidi likiwamo la Tanzania kutokuwa na usajili wa biashara bali ina uwezo wa kusajili chombo kikiwamo kampuni na aina ya biashara kama kampuni au jina la kufanyia biashara.

Aidha alisema  kwa Tanzania Bara , Kampuni husajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni, Sura namba 212 ya Sheria za Tanzania yenye sifa za utu wa kisheria na kufanywa kuwa muendelezo wa kuwapo.

Akifungua mafunzo hayo , Ofisa biashara mkoa wa Morogoro , Gerhard Haule aliwaasa wafanyabiashara mkoani hapa, kuacha tabia ya kuwa na kampuni hewa au za mifukoniambazo alidai  haliwezi  kuwaletea matunda mema ya baadaye.

Alisema kwa kupitia mafunzo hayo, wafanyabiashara wenye kampuni au majina ya biashara ambao wanayatumia au hawajayatumiawataona umuhimu na kuanza kuyatumia kutokana na kupatiwa uelewa thabiti juu ya umiliki wa jina la biashara au kampuni na manufaa yake.

Hata hivyo aliwaasa Brela kuendeleza juhudi za uelimishaji wadau nchi nzima mara kwa mara kwani jambo jema husaidia kujenga uhusiano mzuri baina yao na taasisi mbalimbali wanazohudumia kwani sekta binafsi ndiyo mhimili wa uchumi wa nchi.

Tangu mwaka 1990, Serikali ilifanya maboresho na kuonesha kuwa Taasisi zingine serikali zinaweza kujiendesha zenyewe na hivyo kuipunguzia Serikali kuu mzigo na kutenga Taasisi hizo na kuziita wakala wa Serikali ikiwamo Brela iliyokuwa chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger