Home » » ‘Ongezeko la gharama za tiba Moi limebarikiwa na bodi

‘Ongezeko la gharama za tiba Moi limebarikiwa na bodi

Written By Koka Albert on Sunday, May 27, 2012 | 1:39 AM

SIKU moja baada ya  blog hii kuripoti  habari kuhusu kupanda kwa  gharama za matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili , jijini Dar es Salaam (Moi), uongozi wa taasisi hiyo umetoa ufafanuzi na sababu za kupanda kwa gharama hizo.Akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa Moi, Jumaa Almasi, alisema uamuzi huo umefanywa na Bodi ya Moi.

 “Ni kweli kwamba tumepandisha gharama za matibabu, lakini hatuja kurupuka tu na kufanya maamuzi haya, tulikaa na bodi na kukubaliana,” alisema Almasi.Alisema hata hivyo, gharama hazikupandishwa katika maeneo yote ya tiba na kwamba zimepandishwa katika baadhi ya maeneo.


Almasi alisema sababu ya kupandishwa kwa gharama hizo ni pamoja na  kupanda kwa gharama za vifaa vya kutolea huduma za matibabu.
“Taasisi hii imekuwa ikipokea asilimia 70 ya wagonjwa, wengi wao wakiwa ni  majeruhi kutoka sehemu mbalimbali nchini, kwa hiyo tumefanya hivi hili  kuboresha huduma za matibabu,”alisema Almasi.
Akifafanua mchanganuo wa gharama, alisema wagonjwa wa operesheni ambao huko nyuma  walikuwa wakilipa Sh50,000, sasa watalipa  Sh 75,000 wakati wagonjwa wa dharura watalipa Sh10,000.

Huko nyuma wagonjwa wa kundi hilo walikuwa    hawatozwi gharama za matibabu.Ofisa uhusiano huyo alisema gharama za huduma nyingine mengine kama vipimo vya maabara zitabaki kuwa zile zile.

“Gharama hizi ni kwa upande wa wagonjwa wa kawaida tofauti na wale binafsi ambapo wao wanalipa kwa kiwango kikubwa,” alisema Almasi.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger