Home » » Makocha 20 waitakya Yanga

Makocha 20 waitakya Yanga

Written By Koka Albert on Thursday, May 17, 2012 | 11:58 PM

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema umepokea CV 20 kutoka kwa makocha mbalimbali ndani na nje ya nchi wanaotaka nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mserbia, Kosta Papic.
Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa, ameliambia Championi Ijumaa kuwa wamepokea maombi kutoka kwa makocha hao ambapo wanayafanyia kazi ili kuweza kumpata mwenye vigezo kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame.

“Tumepokea CV za makocha 20 kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo Ufaransa, Sweden na na kwinginepo na kuna makocha wengine kutoka hapahapa nchini. Tupo katika mchakato wa kufanya mchujo ili kuweza kumpata kocha mwenye vigezo atakayeweza kuziba nafasi ya Papic kabla ya michuano ya Kagame kuanza,” alisema Mwesigwa.
Katibu huyo aliongeza kuwa kambi ya wachezaji…
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger