Home » » TCRA yatoa ufadhili kwa wanafunzi wanane

TCRA yatoa ufadhili kwa wanafunzi wanane

Written By Koka Albert on Monday, May 14, 2012 | 4:22 AM

Joseph Zablon
WANAFUNZI wanane wa vyuo vikuu tofauti nchini wamepata Tuzo za Masomo ya Juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo yatafadhiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), baada ya kuibuka washindi kufuatia usaili uliofanyika hivi karibuni.

Akizungunmza wakati wa kuwatangaza wanafunzi hao wanaotoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema ni wanafunzi wengi waliomba nafasi hiyo lakini ni wao pekee ndio walioipata.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Nkoma aliwataka wanafunzi hao kuonyesha uwezo wao katika masomo na kuongeza jitihada ili waweze kuleta matokeo tarajiwa ambayo yatakuwa na msaada mkubwa sio kwao pekee bali Taifa kwa ujumla.

“Kasomeni kwa bidii na macho ya watanzania wengi yapo nyuma yenu kwani wanatarajia mtafanya vizuri na kuweza kutanzua changamoto za mawasiliano zinazolikabili Taifa hivi sasa,” alisema na kuongeza kuwa hadi wao kupatikana watendaji wa mamlaka hiyo wamelazimika kufanya kazi ya ziada.

Wanafunzi  hao ambao katika hafla hiyo kila mmoja alitunukiwa komyuta ya mkononi (Laptop), wanaenda kusoma katika vyuo tofauti masomo ya uhandisi wa mawasiliano katika hatua mbalimbali kwani wapo ambao wanaenda kuchukua Shahada za Uzamivu, Uzamili na Shahada ya kwanza ya masuala ya mawasiliano.

Wanafunzi hao walipata nafasi hizo baada ya kutuma maombi ya kuomba tuzo za masomo hayo  baada ya kuona matangazo ambayo yalichapishwa na mamlaka hiyo katika vyombo mbalimbali vya habari na mpango huo endelevu, ndio mara ya kwanza unatekelezwa na mamlaka hiyo.
Mwisho…………….
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger