Home » » Wanachuo walalamikia wenye nyumba Mtwara

Wanachuo walalamikia wenye nyumba Mtwara

Written By Koka Albert on Wednesday, May 23, 2012 | 3:02 AM

Abdallah Bakari,Mtwara
WANAFUNZI wanaosoma Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara(STEMMUCO),wameomba wamiliki wa nyumba katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuacha kuwatoza kodi ya nyumba kwa kichwa badala yake walipie chumba kama ilivyokwa watu wengine wasio wanafunzi.

Ombi hilo limetolewa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho Sadiki Kitandasa, alipoongea na mwandishi wa habari hizi chuoni hapo.

Alisema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakiingia katika migogoro na wamiliki wa nyumba za kupanga kutokana na kushindwa kulipa kodi kubwa wanayotozwa.
“Ndugu yangu kama unavyojua hapa chuoni hatuna hosteli za kutosha wanafunzi wote. Ni lazima baadhi yetu wapange kwenye nyumba za watu binafsi, sasa wanapokwenda huko wanatozwa kodi kwa kichwa badala ya chumba,”alisema Kitandasa akifafanua kuwa:

“Yaani kama mtakuwa wawili au watatu basi kila mmoja atatozwa kodi yake huku wote mkikaa chumba kimoja.”

Alisema kuwa wanafunzi wengi wanasoma chuoni hapo kwa mkopo wa Serikali ambapo mara nyingi huchelewa kupata fedha kutoka Bodi ya Mikopo na wanapowaeleza wamiliki wa nyumba walizopanga hawataki kuelewa, hivyo kusababisha mivutano.

“Unajua hii inatokana na kodi kubwa tunayotozwa, tunashukuru kwa kutupokea na kutupatia hifadhi, lakini wasitukomoe. Mbona wao wenyewe kwa wenyewe wanatozana kodi ya chumba iweje sisi tutozwe kwa kichwa? Tunadhani hii siyo haki ni vema wakabadilika,” alisema Rais huyo.

Mkuu wa chuo hicho Mchungaji Dk Longino Rutagwelera alisema kuwa zaidi ya asilimia 92 ya wanachuo wanaishi nje ya chuo na kwamba w

Chuo kikuu cha Stella Maris ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT kilianza mwaka 2009 kikiwa na mkondo mmoja tu wa shahada ya elimu ili kuandaa walimu wanaokwenda kufundisha katika shule za sekondari.

Chuo hicho sasa kinatoa shahada za Sosholojia na mwaka ujao wa masomo shahada za Biashara na  sheria zitaongezwa ambapo pia kutakuwa na elimu ya vyeti na stashahada katika Kompyuta,biashara na utunzaji wa maktaba.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger