Home » » Profesa Muhongo: Nimekuta ‘madudu’ ya kutisha Tanesco

Profesa Muhongo: Nimekuta ‘madudu’ ya kutisha Tanesco

Written By Koka Albert on Monday, May 21, 2012 | 2:41 AM

 
Geofrey Nyang’oro
WAZIRI  wa Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo amemkaanga mtangulize wake akisema baadhi ya madudu aliyoyakuta katika wizara hiyo ni makubwa ambayo hawezi kuyasema hadharani.
Profesa Muhongo ni miongoni mwa Mawaziri wapywa walioteuliwa Mei 3, mwaka huu kushika wadhifa katika baraza jipya la mawaziri ambapo kabla ya uteuzi huo aliteuliwa kuwa mbunge kupitia viti maalum na Rais.
Profesa Muhongo mwenye taaluma ya Jiolojia alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akizunguza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika mkutano wao  uliofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wafanya kazi walitaja mambo kadhaa yanayolifanya  shirika hilo kushindwa kujiendesha kuwa ni pamoja na mikataba mibovu iliyoingiwa na Serikali kwa Kampuni ya kufua umeme na vitendo vya baadhi ya watendaji wizarani ambao hujihusisha na hujuma dhidi ya  shirika hilo.

Akijibu hoja mbalimbali za wafanya kazi alisisitiza kuwa, suala la mikataba mibovu iliyoingia na Serikali inajulikana na wananchi wote lakini akasema hata yeye alipoingia wizarani amekuta mambo mabaya ambayo hawezi kuyasema hadharani.

“Ninyi  mnazunguzia mikataba mibovu na mnataka tuifute,wafanyakazi wa Tanesco ni watu waliokwenda shule tuongee vitu vinavyowezekana,ile ni mikataba….siyo kwamba mimi natetea mikataba mibovu yapo mambo niliyoyakuta huku ni makubwa hata mimi siwezi kuyasema hadharani”alisema Muhongo na kuongeza:
“Suala la mikataba huwezi  kulibadilisha kwani imeshatufunga , Serikalini nne zimeingia mikataba,awamu ya kwanza ya pili ya tatu na hata ya nne, sisi katika awamu yetu tunawaahidi hatuwezi kuingia mikataba mibovu ndio sababu nikagusia kuwa mimi kama waziri siwezi kusaini  mkataba wowote unaohusu umeme bila kushirikisha Tanesco,TPDC” alisema Muhongo.

Profesa Muhongo pia alitaja mambo mengine aliyodai ameyakuta wizarani na kuyafanyia kazi katika kipindi kifupi cha siku 18 alizokaa kwenye wadhifa huo kuwa ni pamoja  na suala la uhusiano mbovu baina ya wafanya kazi wa wizara hiyo,Samico, Tanesco na TPDC ambapo kila upande unafanya kazi kivyake na kushutumu upande mwingine.
“Nimekuta hakuna ushirikiano baina ya Wizara,TPDC,Samico na ninyi Tanesco,mbaya zaidi kila upande unatupia lawama upande mwingine,nimenza kwa kulifanyika kazi hilo na kuanzia sasa sisi wote ni timu moja kazi yetu ni kuhakiksha tunatoa huduma bora ya umeme kwa watanzania”alisema Muhongo.
Muhongo alisema yeye ameshaanza kazi na moja ya mambo aliyoyafanya ni kurejesha rasimu ya mapendekezo ya muswada wa kurekebisha sheria  ya umeme iliyokuwa imeandaliwa bila kushirikisha pande zote zinazohusika na masuala ya umeme ikiwamo Tanesco na TPDC.
“Kuanzia sasa pale wizarani kila kitu kitakuwa wazi,mimi sitasaini mkataba wowote bila kuwashirikisha ninyi,sitaruhusu vitendo vya hujuma na mtu yeyote wala kuruhusu kutungwa kwa sheria bila ya kuwashirikisha”alisema Muhongo.
Kuhusu jitihadi za kutafuta  ufumbuzi suala la umeme alisema, kesho Jumanne Maofisa kutoka TPDC,Tanesco na Wazara ya Madini wanatarajia kukutana na Naibu waziri wa Nishati ya umeme , George Simbachewene kujadili na kuandaa mkakati wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini.
Alitaka wataalamu wa umeme kujadili namna ya kulitoa Taifa katika mtindo wa kutegemea chanzo kimoja cha umeme wa maji na badala yake kuangazia vyanzo vingine ambavyo ni makaa ya mawe na gesi.
Pia waziri huyo alitaja vyanzo vingine kuwa ni umeme wa upepo,Jiothramu na jua ambao alisema vyanzo hivi vikitumika vizuri vitalisaidia taifa.
Katika mkutano huo pia  Waziri huoaliwatangazia neema ya kupatikana kwa gesi katika shirika hilo aliposema bombo la kusafirisha gesi linalojengwa kwa sasa ni mali ya serikali.
“Ninachotaka mimi tuache yote yaliyopita kwani tukijikita kushughulika na hayo tunaweza kushindwa kutekeleza hii mipango tuliyojiwekea,hivi sasa bomba la gesi linalojengwa ni mali ya serikali lakini pia Mgodi wa Kiwira taratibu za kuurejesha serikalini zimekamilika na utakuwa chini ya Samico”alisema Muhongo.
Kuhusu mikataba alisema hatua za kufanyia marekebisho mikataba hiyo, zinaendelea ndani ya wizara kama ilivyofanyika kwa ile ya madini ambayo kwa sasa inalipa asilimia 4 ya mirabaha badala ya asilimia tatu ya awali.

Waziri huyo alitaja pia hatua ambazo  wizara imefanya kwa sasa kuwa ni kupitia na  kubaini namna Kampuni zilivyoingia na kufanya kazi ya kusafirisha gesi ambapo alisema, kuna kampuni nyingi zinazofanya kazi hiyo.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger