Home » » Haki za binadamu isiwe kisingizio kukubali ushoga

Haki za binadamu isiwe kisingizio kukubali ushoga

Written By Koka Albert on Friday, May 25, 2012 | 3:22 AM

 Nora Damian
SERIKALI imetahadharishwa kutokubali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu kwa kuwa zinaenda kinyume na maadili. tahadhari hiyo imetolewa na Askofu Charles Gadi wa huduma ya Good News for All Ministry akieleza kuwa licha ya suala hilo kupigiwa debe na mataifa makubwa ikiwemo Uingereza na Marekani ni kinyume na maadili ya Mungu na tamaduni za Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kuliombea taifa katika viwanja vya Biafra, askofu huyo aliitaka Serikali kutokubali vitendo hivyo kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu. “Sisi kama viongozi wa dini tunalaani kwa nguvu zote vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja zinazopigiwa debe na kukubalika katika mataifa makubwa,”alisema Askofu Gadi na kuongeza kuwa:

 “Hata dini hakuna inayokubali ndoa za jinsia moja, ndiyo maana tunaitaka Serikali isikubali kabisa suala hilo,”alisema. Mkutano huo ambao ulishirikisha madhehebu mbalimbali ulikuwa na lengo la kumshukuru Mungu kwa mambo mbalimbali. Katika mkutano huo askofu huyo alisema kuwa ndani ya siku 100 tangu walipoanza maombi, baadhi ya mambo yameanza kufanyika au kujibiwa na Mungu.

Aliyataja baadhi ya mambo kuwa ni taifa kutekeleza kwa vitendo dhana ya utawala bora kwa kuruhusu kujadiliwa kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuanza kushuka kwa bei za vyakula. Alisema kila baada ya siku 100 watakuwa wakifanya tathmini ya mamombi wanayoyafanya ili kuona kama yamejibiwa au la.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger