Home » » Camp Mulla wakali wa muziki kutoka 254 wavunja rekodi kwa kuwa wasanii wa kwanza kutoka Africa Mashariki kushiriki tuzo za BET

Camp Mulla wakali wa muziki kutoka 254 wavunja rekodi kwa kuwa wasanii wa kwanza kutoka Africa Mashariki kushiriki tuzo za BET

Written By Koka Albert on Thursday, May 24, 2012 | 11:33 PM

Camp Mulla
Kundi la wakali wa muziki kutoka 254 Camp Mulla limevunja historia kwa kuwa kundi au wasanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuchaguliwa kushiriki tuzo za BET toka zianzishwe, ambapo wamechaguliwa kushiriki za mwaka huu.

Wakali hawa wamewekwa kwenye Category moja ya International Act Africa Category na wakali wengine kama Lira (South Africa), Whiz Kid (Nigeria), Sakodie (Ghana) na Makobe (Mali).

Camp Mulla wanatarajiwa kusafiri mwezi ujao kwenye utoaji wa tuzo hizo unaofanyika nchini Marekani July 2012, ambapo Nigeria ndio nchi pekee ambayo imewahi kushinda tuzo hizo kupitia kwa D’banj na 2face.
Anaepewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hizo ni Whiz Kid wa Nigeria ambae yuko chini ya lebo ya Akon sasa hivi, hapa ni wakati alipokutana na CP Afrika kusini.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger