Home » » Papic apoteza Matumaini ya Ubingwa

Papic apoteza Matumaini ya Ubingwa

Written By Koka Albert on Thursday, March 15, 2012 | 2:31 AM

 Sweetbert Lukonge
KOCHA Mkuu wa Yanga, Costadin Papic amepoteza matumaini ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza kwenye michezo yao iliyobakia baada kufungiwa kwa muda tofauti tofauti na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia vurugu walizofanya wiki iliyopita katika mechi yao dhidi ya Azam.

Yanga ambayo imebakiza mechi saba ili imalize mbio zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, hivi sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 nyuma ya Azam na Simba ambazo zina pointi 41 kila moja, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Papic alisema hivi sasa ana matuini kidogo kama timu yake inaweza kutetea ubingwa wake kutokana na hali halisi iliyojitokeza hivi karibuni ndani ya klabu hiyo.

Alisema hivi sasa anakabiliwa na kazi ya ziada kuhakikisha kikosi chake kinakaa sawa kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wameathirika kisaikolojia na matatizo yaliyojitokeza hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya baadhi ya nyota wake kumvamia mwamuzi na kumtembezea kichapo.

"Yaliyopita yamepita na sasa tunajipanga kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu zote zilizobakia ingawa nitawakosa baadhi ya wachezaji wangu wa kikosi cha kwanza kwa muda mrefu kutokana na adhabu walizopewa,"alisema Papic.

Alisema,"matumaini ya kutetea ubingwa wetu yapo, ila siwezi kusema tutakuwa mabingwa, tutahakikisha tunapigana na kuweza kutimiza malengo yetu, tutashirikiana kikamilifu, vijana wangu wengine ambao pia nawaamini watafanya vizuri," alisema Papic.

Alisema hivi sasa yupo katika zoezi la kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake ili waweze kusahau yaliyotokea wiki iliyopita na akili zao wazielekeze zaidi katika mechi zao za Ligi Kuu zilizobakia.

Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger