Home » » ‘Waliochakachua leseni wadhibitiwe’

‘Waliochakachua leseni wadhibitiwe’

Written By Koka Albert on Tuesday, March 27, 2012 | 1:45 AM

Gasper Andrew,Singida
SERIKALI mkoani Singida, imeliagiza jeshi la polisi lishirikiane na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ili kuwasaka madereva wote waliochakachua leseni na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone, wakati akifunga semina ya siku moja ya uhamasishaji kwa mafunzo ya (PSV) kwa madereva wa Mkoa wa Singida.

Alisema tabia ya kuchakachua leseni au vyeti, inachangia kwa kiasi kikubwa watu wasiokuwa na sifa kupata kazi za udereva.Alisema watu wasiokuwa na sifa watasababisha kutokea kwa ajali na watu wengi kupoteza maisha.

Dk Kone alisema madereva wa aina hiyo pia wanachangia kwa kiasi kubwa kuchafua fani ya udereva.Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Mkoa, Liana Hassan aliwaangiza pia wamilki wa vyombo vya usafiri, kutokuajiri madereva wasiokuwa na sifa.

"Jengeni utamaduni wa kuajiri madereva waliosoma katika vyuo vya serikali, wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya kuwa dereva, na pia hakikisheni mnaingia mikataba ya ajira na madereva wenu,"alisema Dk Kone.

Pia aliwataka kuyafanyia matengenezo ya kutosha magari na vyombo vingine vya moto ili kuisaidia serikali kupunguza ajali za barabarani.

Awali, Katibu Mkuu wa umoja wa madereva wa mabasi Tanzania, Salum Abdala aliiomba serikali kuwasaka madereva wote wenye leseni zilizochakachuliwa, wakamatwe na kuzuiwa kuendesha magari hadi hapo watakapopata mafunzo stahiki, leseni na vyeti halali.

“Tunawaomba jeshi la polisi, TRA na Takukuru kwa kushirikiana na vyama vya madereva kufanya ukaguzi madhubuti utakaosaidia kuwabaini madereva ambao hawana sifa,” alisema
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger