Home » » Samatta afunika TP Mazembe

Samatta afunika TP Mazembe

Written By Koka Albert on Wednesday, March 7, 2012 | 6:16 AM


KLABU ya TP Mazembe ya DR Congo imetumia mwezi Februari kufanya utafiti kwa wachezaji wake walioitumikia klabu hiyo mwezi huo, huku Mbwana Samatta akiibuka kinara wa kupachika mabao kwa timu hiyo.
Katika utafiti huo uliofanywa na klabu ya TP Mazembe, takwimu zinaonyesha mshambuliaji Mbwana Samatta ameongoza katika kufumania nyavu, ambapo kati ya mabao 15 yaliyofungwa Samata amefunga matano.
Samata amewashinda Luka Lungu aliyefunga manne, Yannick Tusilu amefunga mawili, Treasury Mputu amefunga mawili, Guy Lusadisu amefunga moja na Eric Kanteng amefunga moja pia.
Kwa mujibu wa utafiti huo wa mwezi Februari wa TP Mazembe walitumia wachezaji 31 katika mechi tano, ambapo Samatta, Patrick Ilongo, Joel Kimwaki na Robert Kidiaba waliongoza kwa ubora baada ya kufanya vizuri katika nne mechi kati ya tano walizocheza.
Wachezaji waliofuatia ni Treasury Mputu, Jean Kasusula, Patient Mwepu, Herve Ndonga, Deo Kanda, Yannick Tusilu, Given Singuluma ambao walifanya vizuri katika mechi tatu kati ya mechi tano walizocheza.
Pia, wachezaji Luka Lungu, Treasury Salakiaku, Julio Cesar, Guy Lusadisu, Serge Lofo, Eric na Isaac Nkulukuta Kasongo walicheza vizuri katika mechi mbili kati ya mechi tano walizocheza, huku wachezaji Matampi Ley, Patrick Ochan na Pamphile Mihayo wakicheza vizuri katika mechi moja kati ya mechi tano.
Wachezaji Ilunga Kayanda, Cheiban Traore, Eric Kanteng, Thomas Ulimwengu, Eric Bokanga, Aime Bakula, January Besala, Jerry Kambu, Sheikh Toure na Wissam wenye walikuwa wakiingia kama wachezaji wa akiba.
Katika suala la kutoa pasi za mwisho za ushindi, mchezaji Treasury Mputu aliongoza kwa kutoa pasi sita akifuatiwa na Patrick Ochan pasi mbili, Eric Nkulukuta , Herve Ndonga, Samatta, Serge Lofo, Eric Bokanga, Thomas Ulimwengu na Treasury Salakiaku wote wamepiga pasi moja za mwisho za ushindi.
Kwa jumla,Samatta na Treasury Mputu ndiyo waliofanya vizuri katika takwimu za TP Mazembe, ambapo Samatta aliibuka katika ufungaji na Mputu katika utoaji wa pasi za mwisho za ushindi.
Mchezaji mpya wa timu hiyo Patrick Ilongo naye ameibuka kuwa mchezaji aliyecheza muda mwingi, ambapo katika mechi tano alikosa mechi moja. Amecheza dakika 360.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger