Home » » Tanzania ya mwisho Afrika Mashariki

Tanzania ya mwisho Afrika Mashariki

Written By Koka Albert on Thursday, March 8, 2012 | 3:01 AM

TANZANIA imeporomoka kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 139 mpaka 141 ikiwa imezishinda nchi 64 tu kutoka nafasi ya mwisho kwa mujibu wa viwango vipya vya Shirikisho la Soka la Kimataifa Fifa.
Kwa mujibu wa Fifa, Tanzania imeporomoka baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi mbili zilizopita ambazo ni sare ya bila kufungana DR Congo, na ile ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Msumbiji iliyomalizika pia kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwezi wa pili Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 139 na kabla ya hapo ilikuwa ikishika nafasi ya 137 hivyo inaonyesha kuwa imekuwa ikiporomoka karibu kila mwezi.
Hivi sasa baada ya Tanzania kushika nafasi ya 141 imekuwa ya mwisho katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu Uganda inaongoza ikiwa nafasi ya 88 ikifuatiwa na Rwanda iliyopanda kwa nafasi tatu mpaka nafasi ya 105 na kushika nafasi ya pili Afrika Mashariki.
Kenya imepanda kwa nafasi 10 mpaka kushika nafasi 113 ikiwa ya tatu Afrika Mashariki huku Burundi ikishika nafasi ya nne Afrika Mashariki baada ya kupanda kwa nafasi 11 na kuwa nafasi ya 132 katika viwango vya Fifa.
Kenya na Burundi zimepanda kwa kasi baada ya kushinda mechi zao za kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2013, ambapo Burundi iliichapa 2-1 Zimbabwe huku Kenya ikiichapa pia Togo 2-1.
Tangu kocha Jan Poulsen aanze kuinoa Taifa Stars Agosti 2010, Tanzania imeshika viwango vifuatavyo: Agosti 111, Septemba 111
Oktoba 120, Novemba 124, Desemba 116.
Mwaka 2011: Januari 120, Februari 123, Machi 121, Aprili 112, Mei 117, Juni 127, Julai 127, Agosti 125,Septemba 127, Oktoba 131,
Novemba 136, Desemba 137.
Mwaka 2012: Januari 137, Februari 139 na Machi 141.
Shirikisho la Soka Kimataifa Fifa huwa linatumia viwango hivi katika upangaji wa ratiba za makundi za mashindano wanayoyandaa pia Shirikisho la Soka barani Afrika hutumia viwango hivi kupanga ratiba ya mashindano yake.
Katika upangaji wa ratiba hizo kila kundi huundwa na timu mbili zilizo katika viwango vya juu na timu mbili ambazo zipo katika viwango vya chini.
Katika viwango vipya vya Fifa vilivyotolewa jana Hispania imeendelea kuongoza baada ya kushika namba moja ikifuatiwa na Uholanzi,  Ujerumani, Uruguay, Brazil, England, Ureno, Argentina, Italia na Croatia.
Kwa upande wa nchi za Afrika, timu ya Ivory Coast imeshika nafasi ya 15 katika viwango hivyo vya Fifa na kushika nafasi ya kwanza katika nchi za Afrika ikifuatiwa na Ghana (23), Algeria (35), Zambia (41), Mali (42), Gabon (43), Libya (55), Tunisia (56), Nigeria (57) na Afrika Kusini (60).
Nchi za Afrika ambazo zimeshika nafasi za chini kabisa katika viwango vya Fifa ni Comoro (188), Shelisheli (189), Eritrea (190), Somalia (191), Mauritius (195), Djibouti (197) na Mauritania (203).
Nchi zilizoshika nafasi za mwisho katika viwango vipya vya Fifa ni Anguilla, Bhutan, Brunei Darussalam, Mauritania, Timor-Leste, Andorra, Montserrat, San Marino, Turks na Caicos Islands.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger