Home » » Mamlaka ya hali ya hewa,, yatoa tahadhari,,,,,,

Mamlaka ya hali ya hewa,, yatoa tahadhari,,,,,,

Written By Koka Albert on Wednesday, March 14, 2012 | 1:56 AM

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),  imewatahadharisha wananchi wanaoishi mabondeni kwamba licha ya kupungua kwa kiasi cha mvua katika baadhi ya maeneo nchini, uwezekano wa kunyesha mvua kubwa zinazoambatana na vimbunga ni mkubwa.

Imesema mvua hizo zitakazoambatana na vimbunga zitanyesha kutokana na ongezeko la joto katika Ukanda wa Kusini - Magharibi mwa Bahari ya Hindi huku ikiitaka Taasisi ya Maafa na wadau husika kuanza  maandalizi ya kukabiliana na majanga ya hali ya hewa yanayoweza kutokea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Emmanuel Mpeta alisema,  kutokana na hali hiyo vimbunga vitaongezeka na kusababisha kuongezeka au kupungua kwa mvua katika baadhi ya maeneo  nchini.

“Wanaoishi mabondeni wanatakiwa kuhama kwa kuwa pamoja na kuwa kiwango cha mvua kimepungua lakini kutakuwa na mvua kubwa zitakazoambatana na vimbunga” alisema Dk Mpeta.

Alisema kuwa,  awali walitoa utabiri unaonyesha kuwa kiwango cha mvua kitaongezeka lakini yametokea mabadiliko ambayo yamepunguza kiasi cha mvua cha juu ya wastani kilichotarajiwa, na kuwa cha wastani katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

“Mvua za Masika maeneo ya Kaskazini mwa Tanzania yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, mvua zimeanza kunyesha na zitakuwa za wastani” alisema Dk Mpeta.

Alisema kuwa,  kutokana na mvua hizo kuanza kunyesha vina vya maji katika maziwa, mito na mabwawa vitaongezeka kwa kiasi kidogo.

“Tunazishauri Taasisi za Maafa na Wadau husika,  kuchukua hatua muafaka za maandalizi ya kukabiliana na majanga ya hali ya hewa yanayoweza kutokea” alisema Dk Mpeta.
Share this article :

Post a Comment

KARIBU KATIKA WEBSITE YA KIJANJA, KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA NDANI NA NJE YA NCHI. PIA UTAPATA MAMBO YA ACADEMIC. KARIBU SANA
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. GetInformedTz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger